Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Ahmed Msangi.
Na Emanuel Madafa, Mbeya
Jeshi la Polisi Mkoani Mbeya linamshikilia Lukas Wambura (38) Mkazi wa Banana – Dar es salaam mwenye shahada ya dharura ya kusafiria ab-10044029 akiwa na vipande vinne vya meno yadhaniwayo kuwa ya tembo vyenye uzito wa kilo 8.4 yenye thamani ya dola za kimarekani 30,000, sawa na tshs 64,140,000/=.
Tukio hilo limetokea Novemba 30 -2015 majira ya saa12 jioni katika eneo la custom – mpakani tunduma, , wilaya ya momba Mbeya.
Kamanda wa Polisi Mkoani Mbeya Ahmed Msangi amesema mtuhumiwa huyo alikuwa anavuka mpaka akitokea nchi jirani ya Zambia kuingia nchini na mzigo huo alikuwa ameuficha ndani ya begi lake la nguo.
Wakati huo jeshi hilo la polisi linawashikilia watu wanne kwa kukutwa na silaha mbili pamoja na nyara za serikali.
Kamanda Msangi amewataja watuhumiwa hao kuwani M ohamed Ndilava [55], Mkazi wa Mkwajuni , Nassora Omary [65] Mkazi wa Tabora na Mwanza Mtokambali [39] Mkazi wa Njelenje pamoja na Frank Jonas [32], Mkazi wa Bitimanyanga.
Msangi amesema watuhumiwa hao sita walikamatwa Novemba 30 mwaka huu majira ya saa 3 usiku katika kijiji cha Kapalala Wilayani Chunya Mkoani Mbeya .
Amesema watuhumiwa walikutwa na silaha moja aina ya riffle 416 yenye nambari c.6539833 na gobole moja lisilokuwa na namba, pia walikutwa na nyara za serikali kichwa kimoja cha paa, nyama ya paa na nyama ya sungura vyote vikiwa na thamani ya tshs 1,176,000/=.
Kufuatia matukio hayo Kamanda Msangi anatoa wito kwa yeyote mwenye taarifa juu ya wahalifu wakiwemo majangili kuzitoa katika mamlaka husika ili hatua za kisheria dhidi yao zichukuliwe mara moja.