Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dkt Shaaban Mwinjaka (wa nne kutoka kushoto), akimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni Miliki ya Rasilimali za Reli (RAHCO), Mhandisi Benhadard Tito, wakati akimwelezea namna kiwanda cha kutengenezea breakpad za vichwa vya treni kilivyokuwa kinafanya kazi, na sasa hakifanyi kazi, wakati Katibu Mkuu huyo alipotembelea kiwanda hicho leo asubuhi, Katibu Mkuu ameipa wiki mbili kampuni hiyo na Shirika la Reli Tanzani (TRL) kuuanda timu na kufanya tathmini ya mitambo iliyoharibika na kuhakiki kiwanda hicho kinaanza kufanya kazi.
Jengo ambalo lilikuwa likitumika kama kiwanda cha kutengenezea breakpad za vichwa vya treni, linavyoonekana baada ya kusitisha uzalishaji wa breakpad hizo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dkt. Shaaban Mwinjaka akitoa maelekezo kwa uongozi wa Shirika la Reli Tanzania (TRL), mara baada ya kutembelea eneo la Reli sehemu ya Malindi leo asubuhi.
Reli ambazo hutumika kubadilisha baada ya ziliyopo kuchakaa, zikiwa kwenye eneo la Malindi, kama zilivyokutwa leo asubuhi. (Habari Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikali-Uchukuzi)