Friday, November 27, 2015

Taasisi ya Benjamin William Mkapa yasikitishwa na udanganyifu au utapeli unaoendeshwa na baadhi ya watu wasiojulikana kupitia jina lake



Taasisi ya Benjamin William Mkapa yasikitishwa na udanganyifu au utapeli unaoendeshwa na baadhi ya watu wasiojulikana kupitia jina lake
Taasisi ya Benjamin William Mkapa inasikitika kuwatangazia Umma kwamba kumekuwa na udanganyifu au utapeli unaoendeshwa na baadhi ya watu wasiojulikana wakitumia jina la Taasisi hii katika kutoza fedha watu mbalimbali wakidai kusaidia kupata ajira au ufadhili wa masomo katika sekta ya afya.

Baadhi ya wadanganyifu hao wamekuwa wakitumia barua au akaunti yenye jina "Benjamini Mkapa" katika mtandao wa kijamii wa 'facebook' ambapo huwasiliana na watu, na kuwahadaa kuwa watawapatia ajira au ufadhili baada ya kujaza fomu na kutoa fedha katika mchakato mzima.

Taasisi ya Benjamin William Mkapa (ijulikanayo kama "Benjamin W. Mkapa HIV/AIDS Foundation") inapenda kuwatangazia umma kuwa haihusiki na utaratibu huo wa udanganyifu au utapeli. Tunapenda kuwasisitizia wananchi kwamba hakuna fedha yoyote inayotozwa na Taasisi kwa ajili ya kupata ajira au ufadhili wa masomo chini ya miradi inayoendeshwa na Taasisi yetu.

Kwa mtu yoyote mwenye kutaka kupata habari za uhakika na kamili juu ya masuala hayo, tafadhali, awasiliane na ofisi ya makao makuu iliyopo Dar Es Salaam, na ofisi za Kanda zilizopo Mwanza, Mtwara na Iringa, au kwa kupitia email: info@mkapahivfoundation.org au facebook account: www.facebook.com/BenjaminWilliamMkapaHivAidsFoundation, namba za simu +255 22 2618556-9

Taasisi kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi wanaendelea na uchunguzi ili kuwabaini na hatimaye kuwatia kwenye mikono ya sheria wadanganyifu hao.

Imetolewa na:
Menejimenti ya Taasisi ya Benjamin William Mkapa