Friday, November 27, 2015

ROSE MUHANDO KUNOGESHA TAMASHA LA KUSHUKURU DIAMOND JUBILEE


ROSE MUHANDO KUNOGESHA TAMASHA LA KUSHUKURU DIAMOND JUBILEE

Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion inayoandaa matamasha ya muziki wa injili nchini Bw. Alex Msama akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam wakati alipofafanua mambo mbalimbali kuhusu maandalizi ya tamasha la kushukuru baada ya kufanyika na  kumalizika kwa uchaguzi mkuu wa Tanzania salama salimini.

Msama amesema maandalizi yanaendelea vizuri na amemtangaza rasmi mwimbaji Rose Muhando kama mmoja wa waimbaji wa muziki wa injili watakaoshiriki katika tamasha hilo,  linalotarajiwa kufanyika kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee Desemba 25 na kushirikisha waimbaji wa kimataifa kutoka nchi za Afrika na Ulaya, ambapo ameongeza kwamba mazungumzo bado yanaendelea na waimbaji wengine kutoka nje ya nchi.

Katika picha katikati ni Mwimbaji wa muziki wa Injili Rose Muhando akishiriki katika mkutano huo na kushoto ni William Kapawaga mmoja wa waratibu wa Tamasha hilo kutoka Kampuni ya Msama Promotion.
Mwimbaji wa muziki wa Injili Rose Muhando akiwaelezea waandishi wa habari jinsi alivyojiandaa kutumbuiza katika tamasha hilo la kushukuru, Kulia ni Mkurugenzi wa kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama.
baadhi ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakimsikiliza Mkurugenzi wa kampuni ya Msama Promotion wakati alipokuwa akizungumza nao jijini Dar es salaam kuhusiana na Tamasha hilo.