Wednesday, November 18, 2015

Mtoto wa miaka 7 auawa kinyama, alawitiwa na kunyongwa kisha kutupwa kisimani Yombo vituka




Mtoto wa miaka 7 auawa kinyama, alawitiwa na kunyongwa kisha kutupwa kisimani Yombo vituka
Click image for larger                      version.  Name: 1447841641858.jpg  Views: 1063                       Size: 31.1 KB  ID: 306344

Mwili wa mtoto Joseph kama ulivyokutwa kisimani

Mtoto Joseph mwenye umri wa miaka 7 alikutwa ametupwa katika kisima cha jirani yao usiku wa kuamkia jumatatu tar.16/11/2015, hapa Yombo vituka maarufu kama kwa Chande.

Taarifa za wazazi zinasema mtoto wao walianza kumtafuta usiku saa 2 baada ya kutoonekana nyumbani. Walitembea na kuuliza kila mahali lakini hakukuwa na taarifa za kuonekana kwake. Baadae walitoa taarifa za kupotea kwake katika kituo kidogo cha police Yombo Vituka. 

Usiku huo walijaribu kuangalia katika kisima (ambacho kesho yake alionekana humo) lakini pamoja na kuingiza mti mrefu na kukoroga kwenye maji hakukuwa na dalili za kuwemo kiumbe huyo.

Kesho yake Jumatatu tar. 16/10/2015. Saa 12 alfajiri, mtu mmoja aitwae Kilongola ambae ni jirani alitoa taarifa za kuona kiumbe katika kisima kilekile ambacho walikiangalia usiku.

Ilikuwa ni simanzi kubwa! Baadae police Chang'ombe waliuchukua mwili wa marehemu kwa uchunguzi.

Taarifa zilizopatikana baada ya uchunguzi wa kitaalamu zilionyesha kabla ya kifo chake marehemu alilawitiwa kisha kunyongwa na kutupwa katika kisima kile akiwa amekufa.

Mauaji hayo ya kikatili yanahusishwa na bw.Kilongola ambae ni jirani wa familia hiyo.

Kuna taarifa kwamba marehemu alikutwa akicheza mchezo usiofaa na binti wa Kilongola mwenye miaka 5. Tukio hilo lilishuhudiwa na mke wa Kilongola. Mke huyo hakufurahishwa na kitendo hicho cha Joseph (marehemu) kumfanyia binti yake. Alimchukua hadi kwa wazazi wake na kuwaeleza kitendo alichokuwa anafanya mtoto wao kwa bintiye.

Wazazi wa Joseph walimuadhibu mtoto wao na kumuonya asirudie tena. Waliyazungumza kama wazazi kisha wakayamaliza. Hiyo ilikuwa Jumamosi tar.14/11/2015. 

Bw. Kilongola aliporejea nyumbani na kuelezwa taarifa za kufanyiwa kitu kibaya mtoto wake, hazikumfurahisha na kueleza kutoridhishwa na maamuzi waliyofanya na kusema hayo ni ya kwao yeye atajua cha kufanya.

Kwa sasa bwana Kilongola, mkewe na wazazi wao wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa uchunguzi.

Mwili wa marehemu unasafirishwa kwenda kwao Moshi kwa mazishi.