Saturday, November 14, 2015

DAWA ZISIZOTAKIWA KUTUMIA MTOTO NA HATARI ZAKE‏


DAWA ZISIZOTAKIWA KUTUMIA MTOTO NA HATARI ZAKE‏

istock_medicine_being_poured_into_spoon

Mtoto anapopewa dawa ni muhimu kujua inaanza kutumika kwa kuanzia umri gani ? Kawasabu kuna baadhi ya dawa haziruhusiwi watoto kutumia .Dawa za kifua hairuhusiwi kwa watoto walio chini ya miaka 2. Iwapo mtoto anakifua (kikohozi) chini ya miaka 2 usikimbilie kununua dawa na kumnywesha ni hatari cha muhimu mpeleke hospital .


Madaktari wanashauri dawa ya kifua mtoto aanze kupewa kuanzia miaka 2.

HOME REMEDIES

Asali inafaa kwa matibabu ya kifua  kuanzia miaka 2 na kuendelea kwa kumlambisha mara 2-3 kwa siku ,na kama  mtoto anakifua cha makohozi makali unaweza mtengenezea dawa ya asili  kwa kutumia huu mchanganyiko



Natural-Herbal-Remedies-A-Simple-Treatment-of-Cold2


:CHUNGWA AU NDIMU 1,KITUNGUU SAUMU PUNJE 2,TANGAWIZI KIPANDE KIDOGO,

Jinsi ya kutengeneza: saga kwa pamoja kitunguu saumu punje 2 na tangawizi kipande kidogo. Vikilainika kamulia chungwa koroga na kuchuja kwa  chujio la chai upate  juice ya huo  mchanganyiko .

Tumia kijiko kidogo cha chai kimoja kama kipimo ,utampa mara mbili kwa siku asubuhi na jioni ,anaweza kutapika  makohozi usishtuke ndio njia yake ya kupona.




ASPIRIN

Nidawa hatari kwa mtoto aliechini ya miaka 19,iwapo akapewa  kabla ya miaka hiyo inaweza mletea madhara mwilini. Reye's syndrome ni tatizo linaloshambulia ini na ubongo wa mtoto baada ya kutumia aspirin.

Asprin1

DAWA ZISIZOTAKIWA KUTUMIA MTOTO NA HATARI ZAKE‏

Kuna baadhi ya wazazi wanawapa watoto aspirin ili walale kwa mda mrefu , pale wanapotaka kutoka kwenda sehemu nyakati za usiku ,ni makosa sana pinga na kemea iyo tabia.


USHAURI


Mtoto anapoumwa hakikisha unampa dawa ya mtoto sio ya mtu mzima ,unapokata kipande cha dawa ya mtu mzima na kumpa ni makosa,kama ni pain killer (panadol) basi iwe ya mtoto,dawa ya kifua vile vile kila dawa inakwenda kwa umri. Zingatia kusoma vipimo vya dose epuka kumwo overdose mtoto utamsababishi kifo au maradhi sugu.


SHUKRANI KWA AFYA BORA KWA MTOTO