Wednesday, July 16, 2014

Naibu Waziri wa Uchukuzi atemebelea chuo cha bahari dar es Salaam (DMI)



Naibu Waziri wa Uchukuzi atemebelea chuo cha bahari dar es Salaam (DMI)
Naibu Waziri wa Wizara ya Uchukuzi, Dk. Charles Tizeba akisaini kitabu cha wageni katika ofisi ya Mkuu wa Chuo cha Bahari Dar es Salaam (DMI), mara baaada ya kuwasili chuoni hapo kuangalia shughuli mbalimbali zinazofanywa na chuo hicho na kuongea na wafanyakazi wa Chuo hicho, mwanzoni mwa wiki. Kulia kwake anaemtazama ni Kaimu Mkuu wa Chuo hicho, Kapteni Yasin Songoro.
Mkufunzi wa Chuo cha Bahari Dar es Salaam (DMI), akimpa maelezo ya namna ambavyo wahandisi wanaofanya kazi ndani ya chumba cha injini ndani ya Meli wanavyoendesha mitambo hiyo kwa Naibu Waziri wa Wizara ya Uchukuzi, Dk. Charles Tizeba, wakati alipotembea chuoni hapo mwanzoni mwa wiki kuongea na wafanyakazi wa chuo hicho.
Naibu Waziri wa Wizara ya Uchukuzi, Dk. Charles Tizeba (aliyeweka mikono mfukoni), akimsikiliza Kapteni Peter Mkunja wakati akimpa maelezo ya namna vyombo vya kujiokoa vinavyotumika endapo meli itazama ama kupata hitilafu yoyote, wakati Naibu Waziri huyo alipotembelea Chuo hicho Mwanzoni mwa wiki.
Kaimu Mkuu wa Chuo Cha Bahari Dar es Salaam (DMI), Kapteni Yasin Songoro, akitoa maelezo ya namna ambavyo mashine inayotengeneza vipuri vinayoharibika ndani ya meli inavyofanya kazi kwa Naibu Waziri wa Wizara ya Uchukuzi, Dk. Charles Tizeba, alipotembelea Chuoni hapo Mwanzoni mwa wiki hii.
Sehemu ya Menejimenti na wafanyakazi wa Chuo cha Bahari Dar es Salaam (DMI), wakimsikiliza Naibu Waziri wa Wizara ya Uchukuzi, Dk. Charles Tizeba (Hayupo Pichani), wakati alipoongea nao mwanzoni mwa wiki. (Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Uchukuzi)