Monday, November 16, 2015

BENKI YA BERCLAYS YAWATANGAZA WASHINDI WA AKAUNTI YA MSHAHARA.



BENKI YA BERCLAYS YAWATANGAZA WASHINDI WA AKAUNTI YA MSHAHARA.
BANKI ya Barclays imewazawadia washindi wa droo ya akanti ya mshahara ambayo imechezeshwa mwezi Oktoba mwaka huu ikiwa wamepata washindi watatu ambapo mshindi wa kwanza amepata 100% ya mshahara wake wa kila mwezi, mshindi wa pili amepata 75%  na watatu  50%  ya mshahara wake anaoweka katika akaunti ya benki hiyo.

Washindi hao ni Massoud Ramadhan Lupeja wa Kinondoni jijini Dar es Salaam, Nuran Hatibu Hemed wa  na  Moses Mofati Chilongo.

Hayo yamesemwa na  Mkuu wa Kitengo cha Bidhaa wa Benki ya Barclays, Oscar Mwakyusa  alipokuwa akitangaza washindi wa tatu wa benki hiyo waliojishindia baadhi ya asilimia za akaunti  za mishahara yao.

  Aidha amesema kuwa promosheni ya droo ya mshahara inaendelea kuchezeshwa kwa wenye akaunti za zamani pamoja na watakao fungua akaunti mpya katika benki hiyo.

Kwa upande wake mshindi wa droo iliyochezeshwa leo jijini Dar es Salaam amesema kuwa "Nimefurahi sana kushinda kwa kiwango cha juu pia itasaidia kutatua baadhi ya matatizo yangu."





 Mkuu wa Kitengo cha Bidhaa wa Benki ya Barclays, Oscar Mwakyusa akizungumza katika hafla fupi ya kumkabidhi mshindi wa Droo ya akaunti ya kuweka mshahara wa kila mwezi ambayo inaendelea kuchezwa katika benki hiyo hafla hiyo imefanyika jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Mkurugenzi wa  kitengo cha wateja binafsi wa benki ya Baclyas, Kumaran Pather  na kutoka kulia ni Meneja wa Bidhaa wa benki ya Baclyas, Walence Luteganya na Kaimu mkuu wa kitengo cha masoko wa benki ya Baclyas, Joe Bendera.
Mkurugenzi wa  kitengo cha wateja binafsi wa benki ya Baclyas, Kumaran Pather akimkabidhi msindi wa droo ya akaunti ya kuweka Mshahara katika benki ya Baclyas  ambapo mshindi Massoud Lupeja ambaye amejishindia asilimia 100 ya mshahara wake katika benki hiyo. Hafla hiyo imefanyika leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria katika hafla hiyo ya kumkabidhi mshindi  hundi aliyojishindia, iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo.