Meneja wa Tanesco kituo cha kuzalisha umeme cha Mtera mhandisi Abdallah Ikwasa amewaambia waandishi wa habari waliotembelea kituo hicho kujionea hali halisi ya uzalishaji umeme kuwa hatua hiyo imechukuliwa kutokana na kupungua kwa kina cha maji katika Bwawa hilo hata baada ya kituo hicho kulazimika kuzalisha umeme chini ya mita za ujazo zinazoruhusiwa kitaalam.
Aidha muhandisi Ikwasa amesema kufuatia hali hiyo Kwasasa Tegemeo pekee la nishati ya umeme ni mitambo ya kuzalisha umeme inayotumia gesi asilia ambayo shirika bado linaendelea na hatua za uimarishaji vituo vyake kwa lengo la kuondoa adha ya kukatika kwa umeme katika maeneo yaliyounganishwa kwenye gridi ya taifa.
Chanzo: ITV