Friday, September 18, 2015

VIDEO:Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC) imesema matokeo ya kura za Urais, Ubunge na Udiwani yatabandikwa kwenye kila kituo pale zoezi la kuhesabu litakapokamilika



VIDEO:Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC) imesema matokeo ya kura za Urais, Ubunge na Udiwani yatabandikwa kwenye kila kituo pale zoezi la kuhesabu litakapokamilika
Tume ya Taifa ya Uchaguzi imesema kuwa mwaka huu kura za Rais zitakuwa zinabandikwa kituoni. 

Hatua hiyo imetangazwa rasmi na Mwenyekiti wa Tume Ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Damian Lubuva katika kikao cha mashauriano na Viongozi wa Dini, kilichokuwa kinaongelea, Uhuru, Haki na amani kuelekea Uchaguzi Mkuu wa tarehe 25 Oktoba.

Pia Jaji Lubuva amesema kuwa matokeo yote kuanzia ya Diwani na Ubunge yatabandikwa kituoni pale zoezi la kuhesabu kura litakapokuwa limekamilika.

Jaji Lubuva amesema mwenye mamlaka ya kutangaza kura za jumla za Rais nchi nzima ni makao makuu ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi.

click video hapa chini