Wednesday, September 30, 2015

NEC: HAKUNA WIZI NA UDANGANYIFU WA KURA UCHAGUZI MKUU WA OKTOBA 25



NEC: HAKUNA WIZI NA UDANGANYIFU WA KURA UCHAGUZI MKUU WA OKTOBA 25
 Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi  (NEC), Jaji Damian Lubuva akisalimiana na Mwakilishi wa Chama cha Kitaifa cha Watu Wasioona Zanzibar (ZANAB), Adili Mohamed wakati wa mkutano baina ya taasisi za watu wenye ulemavu nchini na NEC iliyofanyika leo Jumanne Septemba 29, 2015 Jijini Dar es Salaam.
  Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi  (NEC), Jaji Damian Lubuva akisalimiana na Mwakilishi wa Shirikisho la Watu Wenye Ulemavu Tanzania (SHIVYAWATA), Mkoa wa Dar es Salamm Mohamed Chazi  wakati wa mkutano baina ya taasisi za watu wenye ulemavu nchini na NEC iliyofanyika leo Jumanne Septemba 29, 2015 Jijini Dar es Salaam.

Na Ismail Ngayonga MAELEZO
TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC)  imevitoa wasiwasi  vyama vya siasa  kuwa hakutakuwepo na wizi na udanganyifu wa kura katika matokeo ya uchagauzi wa Rais, Wabunge na Madiwani unaotarajia kufanyika nchini tarehe 25 Oktoba, mwaka huu.
AIdha NEC imesema ipo tayari kushirikiana na wataalamu wa vyama hivyo katika kubaini vyanzo vya wizi wa kura iwapo tatizo hilo litajitokeza na hivyo kuhakikisha haki inatendeka kwa vyama vyote vinavyoshiriki uchaguzi huo.

Hayo yamebainishwa leo Jumanne (Septemba 29, 2015) Jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Tume hiyo, Jaji Damian Lubuva wakati wa mkutano wake na wawakilishi wa vyama vya watu wenye ulemavu aliokutana nao kwa ajili ya kupata ushauri na maoni ya taasisi hizo kuelekea uchaguzi mkuu mwezi oktoba mwaka huu.