Daktari mmoja tapeli nchini Kenya, Mugo Wa Wairimu, anayedaiwa kuwabaka wagonjwa wa kike katika kliniki yake amefikishwa mahakamani hii leo jijini nairobi.
Mugo wa wairimu, alifikishwa mbele ya hakimu mwandamizi katika mahakama ya milimani jijini nairobi, , Charity Aluoch baada ya kutiwa mbaroni hiyo jana katika eneo la limuru, alimokuwa amejificha kuwakwepa polisi na Wakenya waliokuwa na ghadhabu.
Mshukiwa huyo anakabiliwa na mashtaka kadhaa yakiwemo kuendesha biashara bila idhini, kujifanya muhudumu wa afya bila vyeti vinavyohitaji na pia tuhuma za kuwabaka wagonjwa wa kike katika hospitali yake mjini Nairobi.
Upande wa mashatakaulifahamisha mahakama hiyo kuwa bado haujakamilisha uchunguzi na kuomba kupewa siku 30 kukamilisha.
Lakini hakimu huyo alisema muda huo ni mrefu na hivo kumwagiza mwendesha mashtaka kukamilisha uchunguzi huo katika kipindi cha siku kumi na nne zijazo.
Mshukiwa huyo sasa anatarajiwa kufikishjwa mahakamani tena tarehe 25 mwezi huu, ila atasalia rumande.
Baadhi ya watu wanaodai kubakwa na muuguzi huyo bandia wameandikisha taarifa kwa polisi.
Muuguzi huyo ambaye inasemekana alikuwa akitoa huduma za matibabu bila idhini, alinaswa kwenye kanda ya video akimdhulumi kingono mgonjwa mmoja katika kliniki yake baada ya kuumpa dawa ya kuwapoteza ufahamu.
Wakenya wa tabaka mbali mbali wameshutumu mshukiwa huyo kwa kutumia nafasi yake kuwadhulumu kina mama ambao walikwenda kwake kupata usaidizi wa kimatibabu, na kutoa wito kwa mahakama kumchukulia hatua kali.
Baada ya kuwa mafichoni kwa siku kadhaa, Wa Wairimu, alikamatwa mjini Limuru hiyo jana katika hoteli moja na nusura aadhibiwe na wenyewe wa eneo hilo waliodai kuwa mshukiwa huyo hafai kuwa miongoni wa jamii.