Matapeli waliotambulika kwa majina ya Innocent Joseph na Kakamba, Iden na Wenzao wawili, wanaotokea Kampuni ya Utafiti ya Research Solution Africa, wamekuwa wakifanya kazi ya kupokea Tenda za Research na watu wamekuwa wakilipwa kwa siku, usiku na mchana ikitegemea na mteja anayefadhili zoezi hilo la utafii.
Mfano miongon mwa benki zinazodhamini ni World Bank ambapo huwa wanawalipa watu kiasi cha Sh. 25,000/= kwa Mkoa wa Dar es Salaam, na iwapo watasafiri mikoani vijini watalipwa kiasi cha Sh. 65,000/=.
Watajwa, hapo juu hivi sasa wanatafutwa kutoka na matukio kadhaa ya kitapeli waliokwisha yafanya siku za hivi karibuni ambapo mwezi uliopita walitangaza tenda ya 'Research Vacancy' na kukusanya wanafunzi wengi tu na wafanyakazi kadhaa waliofika kujiandikisha ili kushiriki mafunzo hayo kwa ajili ya kupewa safari hizo za kwenda kufanya utafiti mikoani.
Watu hao baada ya kujiandikisha walifanyiwa enterview na kama watu 100, hivi wakaambiwa wamechelewa nafasi zimejaa, hivyo wakajengewa mazingira ya utaratibu wa kutoa kitu kidogo, yaani pesa ili kuwawezesha kupata research kwa muda wa miezi mitatu na kupangiwa kulipa kiasi cha Sh. 300, 000/= kwa kila mmoja wao kwa watu 130.
Watu walianza mafunzo na wakaanza kulipwa kiasi cha Sh. 10,000 na kuahidiwa kwenda field kwa muda wa wiki moja baada ya mafunzo hayo.
Baada ya mafunzo watu walipangiwa kwenda kufanya Field katika Mkoa wa Dar es Salaam, Pwani, Bagamoyo, Kibaha na Kijichi for Pilots na wakati wakipangiwa kuondoka juzi kuelekea kuanza field kwamalipo ya Sh.90,000/= kwa siku ambapo malipo yangefanyika kila baada ya siku 10, ambapo kilamwanafunzi baada ya kupiga hesabu aliona kuwa inawalipa kiasi cha kutoona hasara kulipia kiasi cha sh 300,000, 400,000 na 500,000 kwa kila kichwa kulingana na field hitajika.
Watu hao walikuwa wakiendesha mafunzo hayo katika Kumbi za hoteli kubwa kubwa kama Ubungo Plaza,Magomeni na nyinginezo, ambapo watu hawatayari wamekuwa na kundi kubwa lililosambaa hadi mikoani na mafunzo ya mwisho hivi majuzi walifanyia katika ukumbi wa Nguruko uliopo Mbezi Beach, Interchick.
Na katika baadhi ya mikoa kama Morogoro, Arusha na kila Mkutano mmoja wa mafunzo hayo ulikuwa na takriban watu 100 hadi 130, jambo lililowafanya kukusanya jumla ya kiasi cha Sh. milioni 100 hadi 130.
Ilikuwa ni siku ya Ijumaa mida ya saa mbili usiku maeneo ya Mbezi Juu kwa Sanya, kulizuka kundi la viana kama 20, waliovamia nyumba ya mmoja wa matapeli hao na kumkuta mkewe na kumuweka chini ya ulinzi ili apatikane mumewe huyo, aliyetambulika kwa Jina la Innocent Joseph.
Vijana hao baada ya kujieleza kwa wakazi wa eneo hilo baada ya kushukiwa kuwa ni wahalifu, walifafanua na kuelezea mchakato mzima tangua wanachangishwa fedha na kuhudhuria mafunzo hadi siku waliyokimbiwa na kuulizia makazi yake hadi walipofikishwa nyumbani kwake anapopanga.
Baada ya watu hao kufika eneo hilo na kuonyeshwa nyumba anayoishi watu hao walionyesha mshangao mkubwa baada ya kuona nyumba hiyo ambapo wao walihisi kukuta bonge la nyumba na bila kujua kua hata nyumba hiyo pia alikuwa amepanga.
Watu hao walimkuta mkewe na kukaa ndani hapo hadi usiku majira ya saa tano hadi walipofika wakati wa eneo hilo na Mjumbe wa eneo hilo na kuzungumza nao na kugundua kuwa hawakuwa wahalifu bali walikuwa wakidai haki zao na kuomba mikeka ili kukesha nje ya nyumba hiyo kumsubiri mtuhumiwa wao.
watu hao walikesha hadi asubuhi bila mafanikio kwani asubuhi yake walikuwa hata ile familia ya mtuhumiwa wao waliyoikuta usiku tayari ilishatoroka bila kujua ilikopiyia na simu ya mtuhumiwa wao haikupatikana tena na kuamua kuondoka.
Siku ya pili walikuwawatu wengine zaidi ya waliokuja jana yake na kutafuta hadi kupata nyumba ya mtuhumiwa wao na kukuta imefungwa na baadhi yao kuamua kwenda kubomoa mlango na kujisevia baadhi ya vitu kama Flat Screen, Viatu,Sab oofa, Redio na vinginevyo na kusepa navyo.
Namba za matapeli hao ni Aiden 0652213731 na Innocent 0715075807
Shime Watanzania tukomeshe utapeli huu, mtumie kila rafiki yako ili wakamatwe watu hawa.