Wednesday, August 26, 2015

TAMKO LA WAZIRI WA AFYA DKT. SEIF RASHID KUHUSU HALI YA UGONJWA WA KIPINDUPINDU NCHINI


TAMKO LA WAZIRI WA AFYA DKT. SEIF RASHID KUHUSU HALI YA UGONJWA WA KIPINDUPINDU NCHINI
 Waziri wa Afya na Usitawi wa Jamii,Dk Seif Rashid akizungumza na waandishi wa habari hawaponi pichani juu ya Kuepuka kusalimiana kwa kushikana mikono Kunywa maji yaliyo safi na salama – yaliyochemshwa au kutiwa dawa Hakikisha usafi wa mazingira yako wakati wote ikiwa ni pamoja na chooni Kutokula matunda au kitu chochote bila kukisafisha kwa maji safi na salama Kuhakikisha unatumia choo kwa ufasaha na wakati wote Kuwahi mapema na toa taarifa kituo cha huduma  ya afya kilicho karibu na wewe endapo utapatwa na ugonjwa wa kuharisha au kutapika



 Katibu Mkuu wa Wizari wa Afya na Usitawi wa Jamii.Dk Donan Mmbando akizungumza na waandishi wa habari hapo pichani juu ya Usafirishaji holela wa wagonjwa wanaohisiwa kuwa na ugonjwa wa kipindupindu. Ni vyema kutoa taarifa iwapo kuna abiria mwenye dalili  za ugonjwa huu ili ushauri uweze kutolewa wa namna ya kumsafirisha.
 Mwakilishi wa Shilika la Afya Duniani( WHO) Dk Rufaro Chatora akizungumza na waandishi wa habari hapo pichani juu ya  Kufungua kambi za wagonjwa wa kipindupindu katika Manispaa zote tatu za Dar es Salaam ambapo kwa Kinondoni kambi ipo Mburahati, Ilala, kambi ipo kituo cha Afya Buguruni  na Temeke katika Hospitali ya Temeke. Kwa Mkoa wa Morogoro kambi zimefunguliwa Sabasaba na St Thomas.
Waandishi wakimsiliza kwa makini Waziri wa Afya na Usitawi wa Jamii,Dk Seif Rashid.
Picha na Emmanuel Massaka.

IDADI YA WAGONJWA WALIYORIPOTIWA KUAMBUKIZWA NA UGONJWA WA KIPINDUPINDU AMBAO UMELIKUMBA JIJI LA DAR ES SALAAM PAMOJA NA MKOA WA MOROGORO IMEFIKIA WAGONJWA 262  NA VIFO 8.

                                                                                 
Idadi ya wagonjwa waliyoripotiwa kuambukizwa na Ugonjwa wa Kipindipindu ambao umelikumba jiji la Dar es salaam pamoja na Mkoa wa Morogoro imefikia wagonjwa 262,huku vifo  hadi sasa toka ugonjwa huo ugundulike Agost 15 mwaka huu vikifikia nane.

Taarifa hiyo imetolewa leo na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Daktari Seif Rashidi wakati akizungumza nawaandishib wa habari ikiwa lengo ni kutoa taarifa juu ya Ugonjwa huo hatarI ambao umeibuka kwa kasi jijini Dar es salaam pamoja na Mkoani Morogoro.

Aidha alisema kuwa hadi sasa idadi ya wagonjwa katika jiji la Dar es salaam walioambukizwa ni 230 na vifo saba,ambapo Manispaa ya Kinondoni ina wagonjwa 186,Manispaa ya Ilala wagonjwa 22 na Temeke 22 nakwamba wagonjwa waliyolazwa kwenye  kambi  za matibabu ni 71 ambazo ni Mburahati wagonjwa 47,kambi ya Buguruni 15 huku kambi ya Temeke ni wagonjwa 9.

Aliendelea kufafanua kuwa wagonjwa  wengi wamekuwa wakitoka katika maeneo mabalimabali ambapo katika Manispaa ya Kinondoni ni maeneo ya   makumbusho,kimara,Tandale,Manzese,Saranga,Magomeni,Mwananyamala,kibamba,kigogo,Goba,Burahati,Kinondoni na Kijitonyama.

Manispaa ya Ilala ni Buguruni,Majohe,Chanika,Ilala sharif shambana Tabata huku Katika Manispaa ya Temeke wagonjwa wengi ni kutoaka katika maeneo ya kwa Azizi Ally,Keko na Yombo Vituka.


Alisema Mkoani Morogoro wagonjwa waliyoripotiwa Agost 24 mwaka huu ni 32 na kifo kimoja ambapo pia wagonjwa wapatao 15 wamehifadhiwa kwenye kambi ya Matibabu ya Sabasaba Mkoani humo.

Waziri huyo wa Afya na Ustawi wa Jamii ametoa tahadhari kwa jamii kuchukua tahdhari pamoja na kuzingatia kanuni za afya ikiwemo,kuzingatia usafi wa mazingira,kuchemsha maji ya kunywa,kunawa  mikono kwa sabuni kabla na baada ya kula chakula,kuepuka kusalimiana kwa kushikana mikoni,kuzingatia usafi wa vyoo pamoja na kula vyakula ambavyo vimeandaliwa kwenye mazingira safi na salama.

Naye mwakilishi mkazi wa shirika la Afya Duniani Daktari Rufaro Chatora amesema kuwa lazima kuwepo na hatua za haraka za kusafisha visima kwa kemikali maalumu na kuhamasisha jamii kutumia vidonge vya kusafisha maji au kuchemsha maji.

Aidha aliongeza kuwa mamlaka husika zichukue hatua za haraka na madhubuti kushugulikia upatikanaji wa maji safi na salama pamoja na usafi wa mazigira katika maeneo husika nakwamba suala hilo siyo la Wizara ya Afya pekee bali ni ushirikiano na Wadau wengine ikiwemo sekta ya Uchukuzi,Mawasiliano,Maji na Elimu.

Katika hatua nyingine Wizara ya Afya imetoa namba za simu ya mkononi kwa wananchi  ambazo ni 0767300234 ambapo zitatumika kuwasiliana moja kwa moja na mganga mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam ili kupata maelekezo ya kitabibu mara baada ya kuhisi dalili za maambuki ya ugonjwa huo.         


TAMKO LA WAZIRI WA AFYA DKT. SEIF RASHID KUHUSU HALI YA UGONJWA WA KIPINDUPINDU NCHINI