Wednesday, August 05, 2015

Madereva watangaza mgomo mwingine nchi nzima



Madereva watangaza mgomo mwingine nchi nzima

Mgomo mwingine wa madereva nchini Tanzania unanukia  kufuatia Chama cha wafanyakazi madereva Tanzania-TADWU pamoja na wizara ya kazi kushindwa kutekeleza makubaliano yayolifikiwa na tume iliyoundwa na waziri mkuu kutatua mgogoro huo.
 
Kwa mujibu wa naibu katibu mkuu wa TADWU, Bwana Rashidi Salehe amesema kwamba kutokana na Wizara kushindwa kutekeleza makubaliano hayo wanatarajia kugoma tena  kuanzia Agosti tisa mwaka  huu.
 
Amesema  kuwa madereva watagoma tena kufuatia wizara ya  kazi pamoja na Sumatra kuendelea kutumia mikataba ya zamani katika kutoa leseni wakati makubaliano ya tume iliyoundwa na waziri mkuu yalitaka mikataba mipya ianze kutumika kuanzia julai mosi mwaka huu.
 
Katika makubaliano  yao mapya, madereva wa malori yanayotoka nje ya nchi walikuwa wanatakiwa kulipwa mishahara ya shilingi milioni moja, huku madereva wa daladala shilingi laki tano pamoja na posho.