Zahara Muhidin Michuzi akiweka sahihi katika kitabu cha wageni alipowasili katika ofisi za CCM mkoa wa Tabora ili kuchukua form ya kugombea viti maalum kwa vijana.
Binti huyo wa Michuzi mara baada ya kuhitimu elimu yake ya shahada yake ya uchumi UDOM ameona ni vyema akawatumikia wananchi wa nyumbani kwake mkoani Tabora kwa kutangaza nia ya kugombea ubunge wa viti maalum kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi.
Zahara Michuzi (kushoto) na Mwasham Hashim (kulia) karani wa UVCCM Tabora akitoa maelekezo ya uchukuaji wa form hizo.
Zahara Michuzi akikabidhiwa form yake leo katika ofisi za UVCCM mkoa-Tabora
Zahara akiifurahia form yake ya Ubunge wa viti maalum Tabora.
Zahara (kushoto) akilipia fedha ya form hiyo huku mama yake mlezi, Rehema Saidi (katikati), akishuhudia kitendo hicho. Picha na Aloyson Blog wa TBN kanda ya Magharibi.