Na Rahma Khamis Maelezo Zanzibar
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Kwanza wa Rais Mhe. Fatma Abdulhabib Fereji amesema dawa za kulevya ni janga la Kidunia linalopigwa vita na Mataifa yote Duniani.
Hayo ameyaeleza huko Kiwanja cha Kombawapya Zanzibar katika Maaadhimisho ya kupiga vita Utumiaji na Usafirishaji pamoja na Udhalililshaji wa Dawa za kulevya Duniani.
Amesema Zanzibar inakadiriwa kuwa na watumiaji wa dawa za kulevya zaidi ya 9000 idadi ambayo ni kubwa ukilinganisha na visiwa hivyo pamoja na idadi ya wakaazi wake jambo ambalo linahatarisha maisha ya vijana kujiingiza zaidi katika utumiaji huo
Aidha amesema Seikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Tume ya Kitaifa ya Kuratibu na Kudhibiti Dawa za kulevya chini ya Ofisi ya Makamo wa Kwanza wa Rais huadhimisha siku hiyo kila Mwaka kwa lengo la kuitanabahisha Jamii kuwa Dawa hizo ni janga la Kitaifa lisilovumilika hivyo linahitaji nguvu na maarifa ili kupambana na janga hilo.
Hata hivyo Waziri huyo amesema kuwa Zanzibar ni sehemu ya Dunia inayounga mkono juhudi za Mataifa na Jumuiya mbalimbali za Kimataifa katika kupiga vita Dawa hizo ambazo kwa asilimia kubwa zinaathiri nguvu kazi ya Taifa lolote Duniani hasa vijana wenye umri mdogo wakiwemo Wanafunzi.
Waandamanaji katika maadhimisho ya siku ya kupambana na usafirishaji na matumizi ya dawa za kulevya Duniani wakipita mbele ya mgeni rasmi katika kiwanja cha Kombawapya. Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.
Rais wa watoto Tanzania Ameir Haji Khamis akitoa ujumbe wa watoto na dawa za kulevya kwenye sherehe za siku ya kupambana na usafirishaji na matumizi ya dawa za kulevya Duniani katika kiwana cha Kombawapya.
Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Fatma Abdulhabib Ferej akitoa nasaha katika maadhimisho ya siku ya kupambana na usafirishaji na matumizi ya dawa za kulevya Duniani katika kiwanja Kombawapya Mjini Zanzibar.