Wednesday, June 17, 2015

VYAMA VYA WAONGOZA WATALII NA WAPAGAZI TANZANIA WATOA SIKU 30 KWA SERIKALI KUSHUGHULIKIA MADAI YAO



VYAMA VYA WAONGOZA WATALII NA WAPAGAZI TANZANIA WATOA SIKU 30 KWA SERIKALI KUSHUGHULIKIA MADAI YAO
Mwenyekiti wa Chama cha waongoza watalii mkoa wa Kilimanjaro (KGA) Respicius Baitwa akizungumza katika mkutano wa vyama vinayofanya shughuli za Utalii katika hifadhi za taifa juu ya kusudio la kutaka kusitisha kutoa huduma katika hifadhi kutokana na malalamiko yao kutofanyiwa kazi hadi sasa.
Baadhi ya wajumbe walioshiriki mkutano huo uliofanyika katika Hotel ya Uhuru mjini Moshi.
Katibu wa KGA ,James Mong'ateko akizungumza katika mkutano huo.
Wajumbe wengine wa vyama vinayofanya shughuli za utalii katika hifadhi za taifa ikiwemo mlima Kiliamanjaro.
Mwanasheria wa Chama cha waongoza watalii mkoa wa Kilimanjaro (KGA) Elikunda Kipoko akitoa ufafanuzi wa kisheria katika mkutano huo.
Mmoja wa wajumbe katika mkutano huo akichangia hoja juu ya kusudio la kutaka kuhitisha mgomo kwa lengo la kudai maslahi yao.
Mkutano huo ulitoa siku 30 kwa serikali kutekeleza mambo mawili moja likiwa ni kutoa taarifa juu ya kikosi kazi kilichoundwa na mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro ,Leonidas Gama kufuatilia kero mbalimbali ikiwa ni pamoja na kutaka kuonana na waziri wa maliasili na utalii,Lazaro Nyalandu.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.