Duniani saratani ya ziwa ni mojawapo ya saratani inayogunduliwa sana hospitali hutishia uhai wa wanawake na huongoza kwa mauaji kwa wanawake kutokana na Saratani
Katika bara la Amerika saratani ya ziwa ina asilimia 29% kati ya Saratani zote zinazowapata watu pia ni ya pili kwa kusabisha vifo kwa binadamu ikiongozwa na saratani ya mapafu.
Saratani ya ziwa hutokea kwa wanaume pia (bonyeza hapa kuona sratania ya ziwa kwa wanaume)
Saratani ya ziwa mwanzoni huwa haina dalili. Kuhisi maumivu,kuhisi hali mbaya mwilini kutokana na mabadiliko ya mwili mara nyingi sio dalili zake. Saratani hii huweza kutambuliwa kwa kipimo kinachoitwa mamogram ambacho huweza kutambua kabla ya mtu mwenyewe kuona dalili au dakitari kuweza kugundua kwa vipimo vya awali vya kuchunguza ziwa hivyo upimaji wa Afya yako huwa ni wa umuhimu kila baada ya muda Fulani ili kuona mabadiliko ya ziwa.
Kuongezeka uelewa kuhusu saratani ya ziwa kumepelekea kutambulika mapema zaidi kwa sababu wanawake wanapima na kuanzishiwa matibabu wanapokutwa na tatizo hili
Nini hutokea kwenye ziwa mpaka kupata saratani?
Kwa sasa inajulikana kwamba kuna mabadiliko ya tabia ya chembe hai za ziwa yanayosababisha chembe hizi kupata tabia isiyo ya asili ya kuzaliana pasipo kudhibitiwa/kidhibiti
Nini ni vihatarishi vya saratani hii?
Mambo mengi yanahusishwa kusababisha saratani hii zikiwemo sababu za kimazingira,umri, jinsia, dawa na chakula na aina ya jamii Fulani
Umri na jinsia
- Kuwa na umri mkubwa na jinsia ya kike ni kihatarishi ( saratani hii ni nadra sana kutokea chini ya miaka 40)
Tafiti zinaonesha kati ya wanawake 100,000 chini ya miaka 50, 44 hupata saratani hii na hivo hivo walio juu ya miaka 50, 345 hupata Saratani hii (kutoka mediscape)
Historia ya saratani kwenye familia
- Ikiwa una ndugu wa damu, mama au dada yako aliwahipata saratani ya ziwa basi hatari ya kupata mwana familia mwingine inaongezeka—hii inaonyesha kwamba saratani hii hurithiwa kutoka mtoto hadi mtoto. Tafiti zinaonyesha kuwa ikiwa ndugu anahistoria ya saratani ya mayai ya kike basi anauwezekano wa kupata saratani hii au ndugu zake kama si yeye
Masuala ya uzazi na vichochezi mwili (hormones)
- Kuchelewa kupata mimba ya kwanza, kutozaa kabisa, kupevuka (kuanza hedhi mapema) mapema, na kuchelewa kukoma/kusimama kwa mzunguko wa hedhi(menopouse) uzeeni huhusishwa sana kupelekea saratani hii
Historia ya saratani ya ziwa au matatizo mengine kwenye ziwa
- Ikiwa umepata saratani kwenye ziwa moja na likaondolewa mapema, uwezekano wa kupata saratani kwenye ziwa lingine unaongezeka.Magonjwa mengine ya ziwa yanayosemekana kuhusiano na saratani hii ni kama fibroadenoma- ni uvimbe kwenye ziwa usio saratani
Sababu za kimazingira na kimaisha
- Matumizi ya vyakula kama ilivyo kwa saratani ya matumbo (colon n.k) huhusiana sana na saratani hii—chakula chenye wanga kidogo matunda na mboga za majani kwa wingi, mafuta yasiyo na lehamu(cholesterol) mbaya, vyakula vyenye kalori kidogo na pombe kwa kiasi vimeonyesha kuwa huweza kuzuia kupata saratani hii
Uzito kupita kiasi/Kitumbo(obesity)
Uzito kupita kiasi unahusishwa kama ifuatavyo
- Kuwa na zaidi ya kilo 20-25 ya uzito wake wa kawaida kwa Mtu aliye na zaidi ya miaka 18
Dalili zipi zinampata mtu mwenye saratani ya ziwa?
- Mabadiliko kwenye ziwa (kuongezeka ukubwa)
- Ngozi ya ziwa kupata vishimo (dimples) au ziwa kuwa na vishimo kama chungwa
- Vidonda/kidonda kwenye kilembwa cha ziwa
- Kutokwa na uchafu au damu kwenye kilembwa cha ziwa
- Kuvimba mitoki ya kwapani
- Uvimbe mpya ndani ya ziwa unakua mgumu ukishika na usio na umbo la kawaida, viuvimbe vingi na pia ziwa hutofautiana na lenzake
- Ziwa kujishikiza kwenye kuta za kifua ( bonyeza hapa kuandgalia jinsi ya kijipima ziwa lako
Dalili za kuonesha kwamba saratani hii imesambaa ni zipi?
- Kushindwa kupumua vyema(kupumua kwa shida—saratani imeenea kwenye mapafu
- Maumivu ya mifupa- saratani imeenea kwenye mifupa
- Kuongezeka kwa kalisium mwilini
- Kuvimba tumbo
Matibabu ya saratani hii yakoje?
Yapo matibabu ya aina tofauti na hutegemea hali ya mgonjwa na kusambaa kwa saratani hii
Matibabu ya upasuaji kuondoa ziwa lililoathilika endapo saratani haijazambaa sehemu kubwa--mwanamke huweza kuwekewa ziwa bandia kwa ajiri ya urembo
Matibabu ya dawa za chemotherapy na mionzi pia hufanyika endapo saratani imesambaa sehemu nyingine mwilini
Jinsi ya Kujichunguza ziwa:
Wanawake wote wanashauriwa kujichunguza ziwa mara moja au mbili katika mwezi
Uchunguzi wa ziwa sio lazima uende hospitali na dakitari akaona kunauvimbe au mabadiliko, inashauriwa kuanza mwenyewe nyumbani kwani ni rahisi na kwa kufanya hivi unapata faida ya kujua kama kuna mabadiliko katika ziwa lako;
Uchunguzi wa ziwa tunaweza kuugawa katika sehemu mbalimbali
- ukiwa unaoga
- ukiwa umelala
- Ukiwa umesimama mbele ya kioo
Sehemu zote hizi unatakiwa kugundua kama kuna mabadiliko yoyote yale ya rangi, umbo, kuongezeka ukubwa hasa ziwa moja au kupata dimple au vijishimo(dimples). uchunguzi huu unatakiwa kufanywa kwenye mazima yote
Ukiwa mbele ya kioo kama kwenye picha namba 1(chini ya maelezo) ukiwa umesimama angalia kama kuna mabailiko ya rangi umbo/ukubwa kisha nyanyua mikono juu ya kichwa (2) uangalie kama kuna vijishimo vinajitokeza kwenye titi lako (dimples) au yanatofauiana ukubwa na jinsi yanavyojongea unaponyanyua mikono na baada ya hapo nyanyua mkono mmoja juu kama kwenye picha namba 4 na mwingine uwe unapapasa kwa kwa vidole vyako vinne ukipapasa kuanzia katkati ya ziwa kutoka nnje na rudia hivi ziwa jingine kuangalia kama kuna uvumbe ambao haukuwepo na pia papasa sehemu za kwapa na ingia nani zaii uone kama kumevimba mitoki ya sehemu hii aina hii ya uchunguzi unaweza kuufanya ukiwa bafuni wakati unaoga kwani hauhitaji kuwa mbele ya kioo.
Weka mikono kiunoni na ukiwa unaikandamiza kiunoni basi angalia mabadiliko ya umbo, ukubwa kama kwenye picha namba 3. Pia ukiwa umelala na mkono mmoja ukiwa chini ya kichwa (6) basi papasa kuanzia katikatti kwa mduara wa kutoka katikati kwena nnje ya ziwa
baada ya hapo unaweza kuangalia chuchu zako kwa kuuzibana kwa vidole viwii kama picha namba 5 na uangalie endapo kuna usaa unatoka
kumbuka; endapo kunamabaddiliko yoyote kwenye ziwa lako basi mwone dakitari kwa uchunguzi zaidi
pia wanawake wanatakiwa kuwa na tabia ya kuchunguzwa maziwa ili kugundua kama kuna mabadiliko na kwa kipimo kinachoitwa mammogramu kinaweza kutambua mabadiliko hata kama hayanekani kwa kujichunguza mwenyewe.