Athari ya mvua hasa kwa miundo mbinu ni kubwa,pichani ni sehemu ya barabara ya mbezi chini ikiwa imekatika kufuatia mvua kubwa ilionyesha siku nzima ya jana.
Uchafu mkubwa uliokuwa umeziba daraja la mto mbezi chini ukiondolewa baada ya maji ya mto huo yaliyokuwa yakitiririka kwa kazi,kuziba kwa daraja hilo ilipelekea maji ya mto huo kupita juu ya daraja na kupelekea adha kubwa kwa wakazi wa eneo hilo na sehemu nyingine.
Athari kubwa ya mvua iliyopelekea kuleta adha kubwa katikati ya jiji la Dar na kwingineko.Pichani ni hali halisi ya maji kutuama mbele ya soko la Mboga mboga na Matunda eneo la Afrika Sana-Sinza,kufuatia mitaro ya eneo hilo kuzibwa na uchafu.
Pichani mkazi wa Bamaga akitazama athari ya mvua kubwa ilionyesha siku nzima ya jana jijini Dar
Soko la Mwenge nalo ilikuwa ni vigumu biashara kufanyika.
Kufa kufaaaana.
Sehemu ya Mto mbezi
Huyu jamaa sijui alikuwa anatafuta nini
Picha/Habari-Michuzi Media