WAZIRI wa Ulinzi wa Korea ya Kaskazini, Hyon Yong-Chol, ameuawa kwa kupigwa na bunduki ya kutungulia ndege aina ya ZPU-4 kwa kusinzia kwenye hafla ya kijeshi. Waziri huyo aliuawa kutokana na amri ya kiongozi wa nchi hiyo, Kim Jong-Un.
Hyon aliuawa mbele ya mamia ya maofisa wa serikali na jeshi katika kambi moja mjini Pyongyang tarehe 30 Aprili mwaka huu ambapo aliyemuua alisimama umbali wa futi 100 tu akitumia bunduki hiyo ambayo inaweza kufika umbali wa futi 26,000.
Bunduki ya kutungulia ndege aina ya ZPU-4 iliyotumika kumuua Hyon.
Sababu nyingine iliyomfanya waziri huyo aliyekuwa na umri wa miaka 66 na aliyekuwa kiongozi wa jeshi la nchi hiyo tangu mwaka 2012 auawe, ni kutoa kauli za kumpinga kiongozi wa nchi hiyo, Kim Jong-Un katika matukio kadhaa.Hyon aliuawa mbele ya mamia ya maofisa wa serikali na jeshi katika kambi moja mjini Pyongyang tarehe 30 Aprili mwaka huu ambapo aliyemuua alisimama umbali wa futi 100 tu akitumia bunduki hiyo ambayo inaweza kufika umbali wa futi 26,000.
Hyon (kulia) alichaguliwa mwaka 2012 kuwa Waziri wa Ulinzi wa Korea ya Kaskazini.
Uchunguzi umeonyesha kwamba watu wengi waliuawa kwa kutumia njia hiyo ya kikatili katika kambi hiyo mwezi Oktoba mwaka jana.