Wednesday, May 20, 2015

CCM YASUSA MKUTANO WA AMANI


CCM YASUSA MKUTANO WA AMANI

Chama Cha Mapinduzi (CCM) 'kimekacha' kuhudhuria mkutano wa mashauriano kuhusu amani, umoja, utulivu wa nchi na mshikamano, licha ya kualikwa na Taasisi ya Mwalimu Nyerere (MNF). Mkutano huo uliowakusanya pamoja viongozi wa serikali, siasa, dini na wazee maarufu na wastaafu kutoka maeneo mbalimbali nchini, uliandaliwa na MNF na kufanyika jijini Dar es Salaam jana. Mkurugenzi Mtendaji wa MNF, Joseph Butiku, alisema viongozi hao walialikwa, lakini hawakuhudhuria bila kueleza sababu za kutohudhuria, licha ya kupewa mwaliko huo mapema. Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia, alisema
"Ni hulka ya vyama tawala Afrika kusubiri matatizo yatokee ndipo wakae pamoja na wakati huo madhara makubwa yameshatokea...tulitaraji viongozi wa serikali na chama tawala wangekuja tujadili na kuwa na kauli ya pamoja," alisema Mbatia.
Mwenyekiti wa (CUF), Prof. Ibrahim Lipumba, alisema amesikitishwa na CCM kutoonekana katika mkutano huo.
Nini ungependa kukishauri Chama cha Mapinduzi (CCM)?