Wednesday, April 08, 2015

Wadau bandari wazitaka benki kufanya kazi saa 24..... Port stakeholders requires banks to operate at 24




Wadau bandari wazitaka benki kufanya kazi saa 24..... Port stakeholders requires banks to operate at 24
Acting Director General of the TPA, Awadh Massawe.

Financial Institutions in zimetakiwa go with the pace of change in the port of Dar es Salaam to Its offer efficient services at port 24 for Operations.
 
These recommendations were made by stakeholders in Tanzania Ports Management Authority (TPA) to the Financial Institutions in Dar es Salaam.

Taasisi za fedha nchini zimetakiwa kwenda na kasi ya mabadiliko katika Bandari ya Dar es Salaam kwa kutoa huduma zake saa 24 ili kuleta ufanisi katika shughuli za bandari.
 
Mapendekezo hayo yalitolewa na wadau wa Mamlaka ya Usimamizi Bandari Tanzania (TPA) kwa taasisi hizo za fedha jijini Dar es Salaam.
 
Akisoma mapendekezo ya kamati ya vikao vya wadau wa mamalaka hiyo, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Awadh Massawe, ambaye pia ni Mwenyekiti wa vikao hivyo alisema benki nchini zifikirie kuanza kutoa huduma kwa saa 24 ili kuongeza ufanisi wa Bandari ya Dar es Salaam.
 
"Bandari hii ya Dar es Salaam inahudumia mizigo ya ndani na nje kwa saa 24. Ingekuwa vyema kama benki nazo zingeanza kufanya hivyo," alisema.
 
Alisema malipo mengi ya mizigo inayoingia na kutoka katika bandari hiyo yanafanyika kwa njia ya benki, hivyo ni muhimu sasa kuangalia namna ya kuongeza muda wa kazi wa vyombo hivyo vya fedha ambavyo vingi hufunga kazi saa 10:00 au saa 12:00 jioni.
"Jambo hili linachangia ucheleweshaji wa mizigo inayosubiri kulipiwa ili itolewe bandarini," alisema.
 
Aliongeza: "Huduma hii ya benki ni muhimu kufanyika kwa saa zote ili kuirahisishia bandari ambayo inatumiwa na mataifa mengi." 
 
Pia alisema katika kutaka kuondoa kero hiyo, kamati imepanga kikao cha Mei, mwaka huu kuwaalika maofisa wa Benki Kuu Tanzania (BoT) na wawakilishi wa benki zote ili kupata njia ya kutatua changamoto hiyo.
 
Kamati hiyo ya wadau pia ilitumia kikao hicho kuchagua uongozi ambapo Rais wa Chama cha Wakala wa Mizigo Tanzania (Taffa), Stephene Ngatunga, alichaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa kamati ya vikao wa wadau wa TPA. 
 
Sekretarieti inaundwa na wadau wa pande zote mbili za uongozi wa TPA na wadau kwa upande mwingine. Kamati hiyo itakuwa na jukumu la kuratibu na kuendesha mikutano hiyo na kuhakikisha kuwa mambo wanayokubaliana yanatekelezwa.
 
Naye Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Wamiliki wa Malori Tanzania (Tatoa), Elias Lukumay, alikumbusha kuwa Tanzania iko katika ushindani mkubwa katika sekta ya huduma bandari na kuwataka wadau wa mikutano hiyo kuzingatia maslahi ya taifa muda wote. "Ni lazima sisi kama wadau, tuisaidie bandari hii iwe bora ili kuvutia zaidi wateja," alisema.
 
TPA na wadau wake wamekubaliana kuwa na mkutano kila Alhamis ya mwisho wa kila mwezi ili kuangalia na kufuatilia utekelezaji wa mambo wanayobaliana kwa lengo la kuleta ufanisi wa Bandari ya Dar es Salaam.
 
Mbali ya mizigo ya ndani, Bandari ya Dar es Salaam inahudumia nchi saba katika ukanda wa Afrika zikiwamo Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Zambia, Uganda, Rwanda, Burundi, Malawi na Zimbabwe.
 
Baadhi ya wadau waliohudhuria mkutano huo ni pamoja na kampuni za meli, wamiliki wa bandari kavu, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Chama cha Wakala wa Mizigo (Taffa), Jeshi la Polisi, Chama cha Waingizaji wa Mafuta na vitengo mbalimbali vya serikali.