Monday, April 20, 2015

TEMEKE KUINGIA KWENYE FAINALI YA SHIKA NDINGA YA 93.7 EFM




TEMEKE KUINGIA KWENYE FAINALI YA SHIKA NDINGA YA 93.7 EFM
Pichani ni uwanja wa Mwembe Yanga Temeke wakati wa  Shindano la Shika ndinga ya 93.7 EFM.
Shindano la Shika ndinga ya 93.7 EFM kwa wilaya ya temeke limefanyika leo tarehe 18 mwezi wa nne mwaka 2015 ambapo washiriki kumi kutoka wilaya hiyo wamefuzu kuingia fainali ya shika ndinga kwa mkoa wa Dar-es-salaam kati yao watano wakiwa wanawake na wengine watano ni wanaume.Shindano hili kwa wilaya hii lilikuwa la aina yake ukilinganisha na wilaya zingine kwa maaana washiriki walishika ndinga huku mvua kubwa ikinyesha jambo ambalo liliongeza ushindani baina yao.
Shika ndinga ni shindano la aina yake linaloandaliwa na redio ya 93.7 EFM kama namna ya  kutoa shukurani kwa wasikilizaji kwa ushirikiano wao ndani ya mwaka mmoja tangu kuanzishwa kwa redio hiyo ,ambapo washiriki wanatakiwakusikiliza redio ya EFM na kujibu maswali mbalimbali kuhusiana na redio hiyo ili kupata nafasi ya kushika ndinga ya gari ya biashara inayojulikana kama kirikuu kwa muda uliopangwa bila kutikisika, kuyumba ama kutetemeka na mshindi kujishindia gari hiyo ya biashara.
Mchakato wa shindano nzima ulikuwa hivi, wanaume walishika  ndinga  moja na wanawake pia walishika ndinga moja wakiwa wamesimama kwa miguu miwili kwa masaa kadhaa na badae walishika ndinga wakiwa wamesimama na mguu mmoja na hatimaye watano katika kila kundi walifanikiwa kuingia kwenye fainali ambayo itawahusisha washindi wa shika ndinga wa wilaya zote tatu yani ilala , kinondoni na temeke ambao kwa pamoja watashindana kujishindia ndinga ya biashara .
fainali ya shika ndinga itafanyika jumapili ya tarehe 26 mwezi huu wa nne hivo watu wengi wajitokeze ili kushuhudia shindano hili la aina yake.