Tuesday, April 07, 2015

Serikali kwa kushirikiana na viongozi wa kidini wamefanikiwa kupunguza Migogoro ya wakulima na wafugaji,Tanga.


Serikali kwa kushirikiana na viongozi wa kidini wamefanikiwa kupunguza Migogoro ya wakulima na wafugaji,Tanga.
Serikali kwa kushirikiana na viongozi wa kidini, kimila wa jamii ya wafugaji wamefanikiwa kupunguza migogoro baina ya wakulima na wafugaji katika wilaya za kilindi na handeni kufuatia watu zaidi ya 8 kutoka pande hizo mbili kuuawa kwa nyakati tofauti katika kipindi cha mwaka jana kufuatia mapigano ya kugombea maeneo.
Wakizungumza katika mkutano mkubwa uliohudhuriwa na mkuu wa mkoa wa Tanga Bwana Magalula Saidi Magalula na kuhusisha wafugaji zaidi ya 5000 kutoka vijiji mbali mbali kuhusu changamoto zinazowakabili jamii ya wafugaji pamoja na uzinduzi wa kanisa, viongozi wa jamii ya wafugaji wanaojulikana kwa jina la ''Leigwenani'' wameishukuru serikali kwa kuwahusisha katika zoezi la kutafuta suluhu kwa sababu jamii hiyo inaitikia agizo la viongozi wa kimila kuliko la serikali.
 
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Handeni Bi,Husna Rajab amewasisitiza wakulima na wafugaji kutilia mkazo suala zima la amani kwa sababu ndio pekee inayowapa fursa ya kufuga na kuhama maeneo tofauti hapa nchini hivyo amewataka kudumisha amani ili waweze kuwapeleka watoto wao shule. 
 
Kufuatia hatua hiyo mkuu wa mkoa wa Tanga Bwana Magalula Said Magalula amewataka viongozi wa jamii ya wafugaji ''Maleigwenani'' kuhakikisha wanasimamia vyema makundi hayo mawili kwa kusuluhisha migogoro baina yao na akatoa angalizo kuwa ni lazima zoezi hilo liende pamoja na kuhimiza wazazi kuwapeleka watoto wao shule na serikali itahakikisha kuwa vyumba vya madarasa vinajengwa katika maeneo yao.