Friday, April 10, 2015

Rais Kikwete amesema matatizo ya udumavu kwa baadhi ya watoto nchini kunatokana na kutozingatia kanuni za lishe.



Rais Kikwete amesema matatizo ya udumavu kwa baadhi ya watoto nchini kunatokana na kutozingatia kanuni za lishe.
Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Mh Dr Jakaya Kikwete amesema matatizo ya udumavu, kuwa na uzito kidogo kuliko umri na kutokuwa na afya njema kwa baadhi ya watoto nchini kunatokana na kutozingatia kanuni za lishe kutokana na wengi wa wananchi kuangalia zaidi suala la kujaza tumbo kwa kutumia aina moja ya chakula.


Rais Kikwete ameyasema hayo jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na timu maalum iliyoteuliwa na katibu mkuu wa umoja wa mataifa Bwana Ban ki Moon kupitia kwa viongozi wa mataifa mbalimbali duniani kwa lengo la kuhamasisha dunia kujali masuala ya lishe iliyopewa jina la Lead Group Schelling up Nutrition na kuongeza kuwa tatizo la lishe duni linatokana na mazoea yaliyojengeka ya kuwa lishe ni kujaza tumbo badala ya kula vyakula vyenye virutubisho vya kutosha kwa ajili ya mwili.
Kwa upande wake naibu waziri wa wizara ya afya na ustawi wa jamii Dr Kebwe Steven Kebwe amesema licha ya bara la Afrika kuwa na ardhi inayozalisha chakula cha kutosha akitolea mfano Tanzania ambayo kwa sasa ina akiba ya chakula cha takribani tani laki tatu bado nchi hizo zinakabiliwa na tatizo la lishe kunakosababisha udumavu kutokana na mazoea ya kula aiana moja ya vyakula na kwamba kwa sasa elimu zaidi inahitajika licha ya tatizo hilo kupungua kwa asilimia 18 ukilinganisha na tafiti za mwaka 2010 ambazo tatizo la lishe lilikuwa ni asilimia 42 na baadhi ya mikoa ikifikia asilimia zaidi ya 50.