Sunday, April 19, 2015

RAIA 10 WA KENYA WAHUKUMIWA MIAKA 6 JELA



RAIA 10 WA KENYA WAHUKUMIWA MIAKA 6 JELA
Ofisa Uhamiaji Shinyanga


……………………………………………………………………………………..
NA Mwandishi wetu,Arusha.
Raia 10 kutoka nchi jirani ya Kenya wamehukumiwa kifungo cha
  kwenda jela miaka 6 na faini ya shilingi 50,000 kila mmoja
  kutokana na kupatikana na hatia ya makosa ya kuishi nchini
  kinyume na sheria huko wilayani Ngorongoro.
  Akizungumza na Fullshangwe Mkuu wa uhamiaji
  mkoani Arusha Ndelema Mwakipesile alisema kuwa wamekuwa
  wakiendesha operesheni wilayani humo na wameweza kuwakamata
  watuhumiwa hao nakuwapandisha kizimbani kwa kutuhumiwa
  wakiishi na kuendesha shughuli za ufugaji wilayani humo.
  Mwakipesile alisema kuwa Operesheni hiyo iliyoendeshwa kwa
  miezi miwili walifanikiwa kuwakamata raia 14 huku 10
  wakifikishwa mahakamani na wanne ni watoto wadogo ambao
  waliwaachia huru na mifugo yao kutokana na kutokuwa na
  sheria ya kuwatia hatiani.
  "Raia wengi wa nchi ya jirani wamekuwa wakiingia wilayani
  humo kufuata malisho na wamekuwa wakiwatumia  wenyeji
  kuwaficha katika maboma yao na kuweza kuendesha maisha yao
  kinyume cha sheria huku wakiwatumia wenyeji kama sehemu ya
  kuhalalisha uraia wao"alisema mkuu huyo wa uhamiaji mkoani
  hapa
  Alisema kuwa Wageni hao wamekuwa wakiwatumia wenyeji wa
  wilaya hiyo kuishi hapa nchini kinyume cha sheria na
  kuwaachia makundi ya mifugo yao kuichunga kwa makubaliano ya
  malipo na wageni hao kufichwa na wenyeji  kwenye maboma
  yao.
  Aidha alisema kuwa changamoto kubwa inayowakabili
  nikutokuwepo na mipaka inayoeleweka suala linalowapa ugumu
  kutambua wahamiaji hao wapo nchini au nchi jirani.
  Mkuu huyo aliwataja wahamiaji hao waliokamatwa na kuhukumiwa
  kuwa ni Olung'utoto Munka,Pemba Long'oi,Ntolei
  Kokonya,Mofu Kangili,James Silandov,Morjoi ole
  Naereda,Saidimo Leninah,Ntoloi Kikonya na Olong'ototi
  Munka.
VIA-FULLSHANGWE BLOG.