Saturday, April 04, 2015

Kova: Tumejipanga Vizuri Kukabiliana Na Ugaidi Au Ujambazi Wa Aina Yoyote


Kova: Tumejipanga Vizuri Kukabiliana Na Ugaidi Au Ujambazi Wa Aina Yoyote

Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limesema limejipanga vizuri kukabiliana na viashiria vya matukio ya kigaidi na ujambazi wa kutumia silaha katika ukanda wa Afrika Mashariki.
 
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna Suleiman Kova, alisema watashirikiana na vyombo mbalimbali vya ulinzi na usalama ili kuhakikisha udhibiti wa matukio ya uhalifu au fujo zinazoweza kujitokeza, hasa katika kipindi hiki cha Sikukuu ya Pasaka.
 
Alivitaja vikundi hivyo kuwa ni Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji, kampuni binafsi za ulinzi, vikosi vya uokoaji wakati wa majanga na vikundi vya ulinzi shirikishi.