Jumla ya watu 103 wamepoteza maisha katika matukio makubwa ya ajali yaliyotokea kwa kipindi cha mwezi mmoja katika maeneo mbalimbali hapa nchini huku idadi ya majeruhi katika ajali hizo ikifikia watu 138 na baadhi ya majeruhi wakibaki na ulemavu wa kudumu.
Watu 103 kupoteza maisha na watu 138 kujeruhiwa ikiwemo wengine kupata ulemavu wa kudumu imetokea kwa kipindi cha mwezi mmoja tu katika maeneo mbalimbali hapa nchini,huku chanzo kikubwa cha ajali hizi zilizopoteza maisha ya watanzania imedaiwa kusababishwa na uzembe wa baadhi ya madereva.
Jeshi la polisi kikosi cha usalama barabarani mbali na kubaini vyanzo vya ajali hizo zilizotokea katika maeneo mbalimbali nchini kwa kutaja kuwa ni uzembe wa baadhi ya madereva,tatizo la mwendo kasi,ubabe wa baadhi ya madereva kwa magari madogo,mkuu wa kikosi cha usalama barabarani Mohamed Mpinga,amelazimika kuweka wazi idadi ya vifo vilivyotokea katika ajali mbalimbali kuanzia mwezi january mwaka huu,ambapo watu wengi wamepoteza maisha.
Baadhi ya wanasheria wamesema kuna udhaifu mkubwa katika sheria inayotumika,kwani licha ya madereva na wamiliki wa mabasi na magari binafsi wakugundulika kusababisha watu kupoteza maisha kutokana na uzembe wao,hakuna sheria kali inayotumika kuwabana mbali na kutozwa faini ndogondogo huku ndugu wa marehemu waliopoteza maisha katika ajali hizo pamoja na majeruhi hasa wale waliachwa na ulemavu wa kudumu wakibaki njia panda bila kupewa fidia yeyote na wamiliki wa vyombo hivyo.