Thursday, March 12, 2015

Zitto Kabwe Asisitiza Kuwa Yeye Ni Mbunge Halali Wa Kigoma Kaskazini.......Asema Hana Taarifa Ya Kuvuliwa Uanachama CHADEMA



Zitto Kabwe Asisitiza Kuwa Yeye Ni Mbunge Halali Wa Kigoma Kaskazini.......Asema Hana Taarifa Ya Kuvuliwa Uanachama CHADEMA

Siku mbili baada ya mahakama kuu kutupilia mbali ombi la mbunge wa Kigoma kaskazini Mh Zitto Kabwe kujadiliwa na vikao vya CHADEMA kuhusu hatma ya uanachama wake na kutakiwa kulipa  gharama za kesi hiyo, mbunge huyo amedai kuzisikia taarifa hizo kupitia mitandao ya kijamii na vyombo vya habari lakini hana taarifa rasmi.
  
Mara baada ya mahakama kutoa uamuzi wake haraka , mwanasheria mkuu wa chama cha demokrasia na maendeleo Chadema, Mh Tundu Lisu alizungumza na vyombo vya habari kuhusu Chadema kutomtambua Mh Zitto kama mwanachama wa chama hicho.

Ili kusikia kauli ya Mh Zitto kuhusu suala hilo Mpekuzi ilifika katika ofisi ndogo za bunge zilizoko jijini Dar es Salaam na kumshuhudia Mh Zitto akiongoza vikao vya kamati ya kudumu ya bunge ya hesabu ya mashirika ya uma PAC ambapo baada ya kumalizika kwa kikao hicho,Zitto alizungumzia maamuzi hayo ya mahakama na Chadema baada ya kuhojiwa na waandishi wa habari.

"Taarifa  hizo  hata  mimi  nimezisikia  mitandaoni  na  katika  vyombo  vya  habari.Sina  taarifa  rasmi  ya  kuvuliwa  uanachama  na  nipo  kazini  kama  mnavyoniona.....

"Hata  kama  chama  kingekuwa  kimeamua  hivyo, bado  kuna  taratibu  za  kufuata. Wanatakiwa  kumwandikia  barua  spika  wa  Bunge  ili  ajiridhishe  juu  ya  maamuzi  hayo  na  kisha  awajibu.

"Pia, maamuzi  ya  kumvua  ubunge  au  uanachama  mtu  flani  hayafanywi  na  mtu  mmoja, ni  lazima  kikao  halali  cha  chama kikae  na  kuamua  hivyo."  Alisema  Zitto  Kabwe