Majaribio makubwa ya chanjo ya ugonjwa hatari wa Ebola, yanapangiwa kuanza hatimaye nchini Liberia.
Matarajio ni kuwa zaidi ya watu elfu thelathini watajitokeza katika zoezi hilo kubwa la majaribio ya chanjo hiyo iliyotengezwa na kampuni mbili za GSK na Merck.
Katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita, zaidi ya watu elfu tisa wamefariki katika mlipuko huo mkubwa wa Ebola.
Mataifa yaliyoathirika magharibi mwa Afrika ni pamoja na Guinea, Sierra Leone na Liberia.