WADAU wote wa Tasnia ya Filamu nchini,wanakumbushwa kuwa mwisho wa kupokea Filamu kwaajili ya Tamasha la Filamu la Nchi za Jahazi (ZIFF) ni Tarehe 31/01/2015 kwa waandaaji filamu wote wa ndani na nje ya nchi.
"Kama wewe ni Mtanzania na unataka kuwasilisha filamu yako basi wasiliana na Ibra Mitawi +255 713 300997 au +255 783 300997 au mnaweza kutuma ofisini Zanzibar moja kwa moja, hatutapokea filamu yeyote baada ya tarehe hiyo".
Tunaomba pia mjaribu kuweka filamu ikiwa ndani ya DVD moja na si Part 1 & 2, iwe kwaajili ya Festival. Na wale ambao wanaweza kuweka filamu zao online basi waingie www.ziff.or.tz na unaweza kusubmit online pia unaweza kutuma link ya YouTube au Vimeo katika filmdept@ziff.or.tz
Nawatakia Heri ya Mwaka Mpya.