Saturday, January 10, 2015

WAZIRI WA NISHATI NA MADINI PROFESA SOSPETER MUHONGO APATA MAPOKEZI MAKUBWA WILAYANI KISHAPU MKOANI SHINYANGA. AITWA “MZEE WA NGUZO” NA KUKABIDHIWA ZAWADI KWA KUSAMBAZA UMEME KWA KASI KUBWA WILAYANI HUMO


WAZIRI WA NISHATI NA MADINI PROFESA SOSPETER MUHONGO APATA MAPOKEZI MAKUBWA WILAYANI KISHAPU MKOANI SHINYANGA. AITWA "MZEE WA NGUZO" NA KUKABIDHIWA ZAWADI KWA KUSAMBAZA UMEME KWA KASI KUBWA WILAYANI HUMO
 Kaimu Mkuu wa Mkoa wa  Shinyanga Anna Rose Nyamubi  (mbele) akizungumza na  Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (kulia)  pamoja na watendaji wake waliomtembelea ofisini kwake kabla  ya kuanza ziara rasmi katika mkoa  wa Shinyanga. Profesa Muhongo anafanya ziara katika mkoa huo kukagua  miradi  ya umeme  inayotekelezwa na  Wakala
 
 Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo akisalimiana na baadhi  ya wakazi wa wilaya ya Kishapu mara baada ya kuwasili wilayani humo. Kushoto ni Mbunge wa Kishapu  Suleiman  Masoud Nchambi
 Wakazi wa  Kata ya  Bubiki  wilayani Kishapu  wakimpokea kwa shangwe Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo mara alipowasili wilayani hapo huku wakiwa na mabango yaliyosomeka " Profesa wa Kweli, Nchi sasa inang'aa vijijini, Wewe ni Jembe".
 Wakazi wa Kata ya  Seke Ididi iliyoko  wilayani Kishapu mkoani Shinyanga wakimlaki kwa nyimbo   Waziri wa Nishati  na Madini Profesa Sospeter Muhongo mara baada ya kuwasili katika kata hiyo.
 Mmoja wa wakinamama kutoka kata ya Igubi  wilayani Kishapu mkoani Shinyanga akimfunga vitambaa mkononi  Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo kama  heshima  kwa kazi kubwa aliyoifanya ya  kusambaza umeme katika kata hiyo. Kata hiyo ni moja  ya kata zinazonufaika na mradi wa umeme vijijini  unaotekelezwa na REA Awamu ya Pili
 Mbunge wa Kishapu Suleiman Masoud Nchambi  (katikati) akijumuika na wakazi wa Kata ya  Igumbi iliyopo  wilayani  Kishapu kucheza ngoma ya kumpongeza Waziri wa Nishati na Madini kwa juhudi zake za kusambaza umeme katika  kata hiyo pamoja na jimbo lake.
 Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (kushoto) na Mbunge wa Kishapu Suleiman Masoud Nchambi  (kulia) wakifuatilia taarifa ya utekelezaji wa miradi ya umeme vijijini inayosimamiwa na REA Awamu ya Pili iliyokuwa inatolewa na Meneja Utaalamu Elekezi kutoka REA Gissima Nyamohanga (hayupo pichani)
 Mtaalamu kutoka kampuni  ya kusambaza umeme  vijijini  ya LTL (PVT) LTD  Michael Marenye (kushoto) akitoa taarifa ya hatua iliyofikiwa ya ujenzi wa miundombinu ya umeme katika wilaya ya KIshapu. Kulia ni Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo.
 Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo akisisitiza jambo alipokuwa akizungumza na wakazi wa Kata ya Mwamalasa wilayani Kishapu.
 Wakazi wa kijiji cha Ndoleleji  wilayani Kishapu wakimsikiliza kwa makini  Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (hayupo pichani). Profesa Muhongo ameahidi kuwapatia umeme kabla  ya tarehe 30 Aprili, mwaka huu.
 Wakazi wa Bubiki wilayani Kishapu wakimkabidhi  Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (kushoto)  zawadi ya mbuzi wawili kama pongezi kwa kazi nzuri  ya kusambaza umeme katika kata hiyo.
 Wakazi wa Kata ya  Seke Ididi wilayani  Kishapu  wakiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (katikati) mara baada ya kumkabidhi  zawadi ya mbuzi wawili kama pongezi kwa kazi nzuri  ya kusambaza umeme katika kata hiyo.
 Mbunge wa Jimbo la Kishapu Suleiman Masoud Nchambi akisisitiza jambo wakati  wa mkutano huo
 Wakazi wa Kata ya Mwamalasa wilayani  Kishapu wakimkabidhi  Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo ( wa tatu kutoka kulia)  zawadi ya mbuzi wawili kama pongezi kwa kazi nzuri  ya kusambaza umeme katika kata hiyo.
Sehemu ya umati wa watu kutoka  Kata  ya Bubiki wakishangilia hotuba ya  Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (hayupo pichani).