Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (katikati) akitoa maelekezo kwa uongozi wa kijiji cha Tura wilayani Uyui mkoani Tabora kuhakikisha umefanya mkutano na wananchi ili kufanya makubaliano jinsi ya kusimamia mradi wa umeme wa kontena ili wananchi waanze kunufaika mara moja.
Mtendaji wa kijiji cha Tura wilayani Uyui mkoani Tabora Gundi Igonzo (kulia aliyevaa koti la kijani) akitoa maelezo juu ya mradi wa umeme wa kontena kijijini hapo mbele ya Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (katikati).
Haji Ally Kuyanga ambaye ni Katibu wa Mbunge (Siasa) Jimbo la Igalula akihamasisha wananchi (hawapo pichani) umuhimu wa mradi wa umeme wa kontena katika kijiji cha Tura wilayani Uyui mkoani Tabora kwenye mkutano wa Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo na wananchi hao.
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (katikati) akitoa maelekezo kwa uongozi wa kampuni ya kusambaza umeme katika wilaya ya Uyui na Mirambo ya Chico – CCC ya China mara baada ya kutembelea eneo palipohifadhiwa vifaa kwa ajili ujenzi wa miundombinu ya umeme katika wilaya za Uyui na Mirambo.
Mtaalamu kutoka Kampuni ya Chico – CCC, Luo Xiaoyong (kulia) akitoa maelezo kwa Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (kushoto) juu ya hatua iliyofikiwa ya utekelezaji wa mradi wa kusambaza umeme katika wilaya za Uyui na Urambo mara Waziri alipotembelea eneo palipohifadhiwa vifaa kwa ajili ya kazi hiyo.
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo akisalimiana na wakazi wa Inala mkoani Tabora kabla ya kufanya mkutano nao ili kusikiliza kero zao.
Sehemu ya umati wa wakazi wa kijiji cha Inala mkoani Tabora wakifuatilia kwa makini hotuba iliyokuwa inatolewa na Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo ( hayupo pichani)
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (kulia) akihutubia wakazi wa kijiji cha Usindi wilayani Kaliua mkoani Tabora.
Mkazi wa kijiji cha Usindi wilayani Kaliua mkoani Tabora Furaha Mgamba (kulia) akiwasilisha hoja mbele ya Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (kushoto) mara Waziri alipofanya mkutano ili kusikiliza kero za wananchi hao.
Kwaya ya Yeriko kutoka Kata ya Songambele wilayani Urambo mkoani Tabora ikitumbuiza wimbo maalumu wa kumpongeza Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo kwa kasi yake kubwa ya kusambaza umeme vijijini pamoja na usimamizi mzuri wa sekta ya madini.
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo akizungumza na wakazi wa kijiji cha Igalula wilayani Uyui mkoani Tabora. Aliyemshikia mwamvuli ni Katibu wake, Joseph Kumburu.