Wednesday, January 14, 2015

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Kazi Maalum) Profesa Mark Mwandosya ametembelea mradi wa ujenzi wa mabwawa Sudan


Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Kazi Maalum) Profesa Mark Mwandosya ametembelea mradi wa ujenzi wa mabwawa Sudan
Kwa mwaliko wa Mheshimiwa Murtaz Musa Aballa Salim,Waziri wa Maji na Umeme wa Jamhuri ya Sudan,Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Kazi Maalum) Profesa Mark Mwandosya ametembelea mradi wa ujenzi wa mabwawa katika mito ya Setit na Upper Atbara,jimbo la Gadaref na jimbo la Kassala nchini Sudan.
Mabwawa haya mawili yanaunganishwa na tuta moja lenye urefu wa km 13. Utakapokamilika Januari 2016 mradi huu utazalisha MW 320 za umeme na maji yatatumika pia kwa kilimo cha umwagiliaji na kuupatia maji mji wa Gadaref.
Waziri Mwandosya na Mama Lucy Mwandosya wawasili na kusalimiana na wahandisi washauri na wajenzi wa mradi.
Waziri Mwandosya,wa 4 kushoto akiwa mble ya kitolo cha maji (spillway) cha bwawa la mto Setit.Wengine katika picha kutoka kushoto ni: Ngusa Izengo,Katibu wa Waziri; Grace Nsanya,Mkurugenzi Msaidizi Wizara ya Maji;Mhandisi Mustafa Hussein,Mshauri wa Ujenzi wa Mabwawa Sudan; Abd El Aziz El Obaid, Afisa Uhusiano,Wizara ya Maji na Umeme,Sudan; na Mama Lucy Mwandosya.
 Waziri Mwandosya na Mama Mwandosya wakitambulishwa kwa Mheshimiwa Hasabu Mohamed Abd El Rahman kwenye hafla ya kuanza kujaza bwawa la Mto Setit na lile la Mto Atbara,
Ujenzi unaoendelea wa mfumo wa kupeleka maji kwenye mashine za umeme
( penstocks ) kwenye mto Upper Atbara
Waziri Mwandosya,kulia,katika picha ya pamoja na Mheshimiwa Hasabu Mohamed Abd El Rahman,Makamu wa Rais wa Sudan ( aliyeshika fimbo) ,na Mheshimiwa Murtaz Musa Abdalla Salim,Waziri wa Maji na Umeme wa Sudan baada ya sherehe za kuzindua kuanza kujaza maji kwenye mabwawa ya Setit na Upper Atbara,