Hii itakuwa rahisi sana mtu wangu, hivi mara ngapi umeshawahi kwenda sehemu ukakutana na maandishi ambayo umeshindwa kuyaelewa?Teknolojia imekuwa msaada kwenye mengi mtu wangu, pata picha unasafiri kwa mara ya kwanza kwenda China, unaingia mgahawani, unapewa menu imeandikwa kichina, unaanzia wapi kwanza? Google wanatusogeza hapa, google translate app itakusaidia kama unayumia smartphone yako unaweka app hiyo halafu unaanza kuitumia, mfano unakutana na bango lenye maandishi unafungua app, unaionyesha camera ya simu kwenye maandishi hayo unapiga picha, kwenye kioo cha simu inakuonyesha maana ya neno hilo!
Mbali na hivyo app hiyo inaweza kukutafsiria kwa sauti hata kile ambacho mtu anakiongea, yenyewe inakupa tafsiri kwa lugha unayotaka.
Ni rahisi tu, hauhitaji kuwa na internet ili uitumie, ni app ambayo inafanya kazi hata kama huna bundle mtu wangu, inapatikana bure kwa wanaotumia android na iPhone pia.