Wachezaji Bao nguli hapa nchini wakioneshana ubingwa katika Tamasha la Kumuenzi aliekuwa Mlezi wa Mchezo huo Hayati Rashidi Mfaume Kawawa.
Rais wa Chama cha Mchezo wa Bao mchini Bw Mandei Likwepa akionesha moja ya barua kwa waandishi wa habari hawapo pichani iliyo andika na aliekuwa Mlezi wa Mchezo huo Hayati Rashidi Mfaume Kawawa enzi za uhai wake.
Mfanya biashara maarufu nchini Bw Mohamed Sharifu akiongea jambo mbele ya wanahabari, wapenzi na wachezaji wa mchezo wa Bao walioudhuria Tamasha hilo.
Wajukuu wa Mzee Kawawa kutoka kushoto ni Mariamu Msemo na wamwisho kulia ni Adam Chacha wakichuana vikali katika mchezo wa Bao walio ucheza katika Tamasha la kumuenzi Hayati Babu yao Mzee Kawawa.
Mjukuu wa Mzee Kawawa Bi Dora Abdala akichuana vikali na mmoja kati ya chezaji nguli wa mchezo huo katika Tamasha la kumuenzi Hayati Babu yao Mzee Kawawa.