Saturday, January 03, 2015

BREAKING NEWS: OFISI ZA ACT ZAPIGWA KOMEO


BREAKING NEWS: OFISI ZA ACT ZAPIGWA KOMEO

Mwenyekiti wa ACT, Lucas Limbu            (kushoto) akiwa na aliyekuwa katibu wake, Samson Mwigamba

Mwenyekiti wa ACT, Lucas Limbu (kushoto) akiwa na aliyekuwa katibu wake, Samson Mwigamba

MWENYEKITI WA CHAMA CHA ACT-TANZANIA, LUCAS LIMBU, AMEZIFUNGA KWA KOMEO, OFISI ZA CHAMA HICHO ZILIZOKO KIJITONYAMA, JIJINI DAR ES SALAAM.

MBALI NA KUZIFUNGA OFISI HIZO, LIMBU AMEMUANDIKIA MKUU WA JESHI LA POLISI KUWA OFISI ZA CHAMA HICHO ZIMEFUNGWA KWA KILE ALICHOITA, "KUZUIA UHALIFU."

Ameongeza, "Yeyote atakayeingia ndani ya ofisi hiyo bila idhini ya mwenyekiti, ni mvamizi na achukuliwe kuwa mhalifu anayetaka kukiibia chama mali zake."
Aidha, Limbu amewasilisha kwa msajili wa vyama vya siasa, nyaraka za uthibitisho wa kufutwa uwanachama Pro. Kitila Mkumbo, aliyekuwa mjumbe wa Kamati Kuu (CC), Samson Mwigamba, aliyekuwa katibu mkuu na Shaban Mambo, aliyekuwa akijitambulisha kuwa makamu mwenyekiti.