Thursday, January 15, 2015

NHIF yaendelea kutoa somo kwa wadau wa afya jijini dar

Mratibu wa Mtandao wa Mfuko wa Afya ya Jamii (TNCHF), Camillius Haule (kulia) akizungumza katika ufunguzi wa Mkutano kati ya Maafisa wa NHIF na wadau wao,juu ya Mpango wa Kikoa (Mutual Plan) unaoratibiwa na Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) uliofanyika leo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Msimbazi Center,Ilala jijini Dar es Salaam.Wengine pichani ni Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Kanda ya Temeke,Ellentruda Mbogoro (wa pili kulia),Afisa Uratibu wa NHIF kutoka Makao Makuu,Catherine Masinjisa pamoja na Afisa Uratibu wa NHIF toka Temeke,Mbali Shitindi. 
Afisa Uratibu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kutoka Makao Makuu,Catherine Masinjisa akitoa somo kwa wadau wa Mfuko huo kuhusu Mpango wa Kikoa (Mutual Plan) unaoratibiwa na Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) uliofanyika leo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Msimbazi Center,Ilala jijini Dar es Salaam.
Mmoja wa wadau wa Mfuko huo,Sunagritha Mapunda akionyesha fomu alizokabidhiwa kwa ajili ya kujiunga na uanachama wa Mfuko huo.
Sehemu ya Wadau wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) wakifatilia mada mbali mbali zilizokuwa zikitolewa kwenye mkutano huo.