Akisoma mashataka yanayomkabili mwenyekiti huyo mbele ya hakimu mkazi wa wilaya ya Dodoma Rebeca Mbili mwendesha mashtaka wa serikali Godfrey Wambali ameiarifu mahakama hiyo kuwa mnamo tarehe 6/9/2014 ukumbi wa chuo cha mipango eneo la miyuji Dodoma mwenyekiti huyo alitenda makosa mawili ambapo kosa la kwanza lilikuwa ni kushawishi kutenda kosa la jinai ambapo ni kinyume na sheria kifungu namba 309 kikisomeka pamoja na kifungu namba 35 cha sheria ya kanuni ya adhabu sura ya 19.
Kosa lingine ni kuzuia ukusanyaji kodi kwa wafanyabiashara kwa kutumia mashine za kielektroniki za EFD ambapo ni kukiuka sheria ya kodi ya mwaka 2004 kifungu namba 107 {c} cha sheria ya kodi sura namba 332.
Mwenyekiti huyo aliyewakilishwa na wakili wa kujitegemea Godfrey Wasonga baada ya kusomewa mashataka yanayomkabili dhamana ilifunguliwa lakini hata hivyo hadi tunaondoka natika viwanja vya mahakama aliamriwa kubaki rumande kutokana na wadhamini kutokidhi vigezo vya dhamana .
Wakati hayo yakiendelea katika mahakama ya hakimu mkazi Dodoma wakazi wa mji huo wamejikuta katika wakati mgumu kufuatia maduka ya bidhaa mbalimbali yaliyoko katikati ya mji kufungwa kutokana na wafanyabiashara hao kuitaka serikali imuachie huru mwenyekiti wao.