Wananchi hao waliokuwa na hasira wamesema hakuna sababu ya kuwa na mwenyekiti ambaye wananchi hawamkubali kwa sababu katika uchaguzi uliopita kulikuwa na udanganyifu katika upigaji kura,kutokana na hali hiyo wamesema ni bora kuachana na vyama vya siasa wachague mwenye kiti wa kimila ili kukisaidia kijiji cha puma kupata maendeleo.
Baada ya vurugu kuongezeka diwani wa kata hiyo kwa tiketi ya CCM,Bwana ramadhani kulungu ilibidi kufunga kikao hicho ili kuweza kumnusuru mwenyekiti wa kijiji cha puma na kuwatuliza wananchi ilikusitokee uvunjifu wa amani.
Mwenyekiti wa kijiji cha puma kwa tiketi ya CCM ,Bwana Sifa Joramu awali ambaye alishindwa kabisa kuendesha kikao chake ,baada ya jeshi la polisi kuingilia kati na kuamua kumsindikiza kwa ulinzi mkali huku wananchi waki mzomea na kusema hawamtaki,amesema hizo ni fujo za vyama vya upinzani lakini yeye atahakikisha kazi anafanya kwa sababu yeye ndiye aliyeshinda na kuapishwa kwa kazi ya uwenyekiti wa kijiji cha puma.
Kundi la watu waliamua kumfuata na kumbeba juu kisha kumzungusha mitaani Bwana Hassan Chaimbo aliye gombea kwa tiketi ya CHADEMA na kushindwa kwa kupata kura mianne arobaini na nne dhidi ya Bwana Sifa Joramu alishinda uwenyekiti wa kijiji cha puma kwa tiketi ya CCM katika uchaguzi uliofanyika mwishoni mwaka jana na kupata kura mianne hamsini na saba.