Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ruvuma Mihayo Msikhela
Kwa mujibu wa kamanda wa polisi wa mkoa wa Ruvuma Mihayo Msikhela amesema mtuhumiwa huyo alikuwa anashikiliwa kituoni hapo kwa tuhuma za kuvunja jingo la polisi na kuiba radio call ya kituo hicho mwaka jana na kisha kutoroka na jeshi lilimsaka na kufanikiwa kukamata na kumuweka mahabusu ili kumfikisha mahakamani kujibu tuhuma zilizokuwa zikimkabili.
Amesema chanzo cha awali kuhusu tukio hilo lililotokea Januari 23 mwaka huu majira ya saa 12 asubuhi mtuhumiwa huyo alisikika akilalamika sana huku akilia na kudai kuwa ndugu zake hawampendi wakati akiongea na wenzake mahabusu walimokuwa wamewekwa.
Kamanda Msikhela amesema mara baada ya askari waliokuwa zamu kumaliza muda wao waliingia wengine na kabla ya kutoka kazini askari hao walikabidhiana kituo pamoja na mali zilizopo kituoni hapo mtuhumiwa huyo pamoja na watuhumiwa wengine watatu wenye makosa tofauti wakiwa mahabusu na ndipo mtuhumiwa Bosco Ndunguru alitumia muda huokutoka na kujifanya akielekea chooni na kuingia chumba cha jirani na mahabusu ambacho kilikuwa hakina mtu na kujitundika kwa kutumia shati.
Amesema aliweza kufanikisha kitendo hicho kwa kujitundika kwa kutumia shati na kwa kujitundika kwenye nondo ya mlango wa chumba hicho mpaka alipogunduliwa na mmoja kati ya watuhumiwa waliokuwepo ndani na kutoa taarifa kwa askari waliokuwa zamu ilipofika saa moja asubhi Januari 24mwaka huu.
Amesema jeshi la polisi kwa kushirikiana na mganga kutoka hospitali ya wilaya ya Mbinga waliufanyia uchunguzi mwili wa marehemu na kukabidhiwa kwa ndugu kwa ajili ya shughuli za mazishi.