Saturday, January 10, 2015

MOTO WATEKETEZA GHALA LA KUHIDHIA RANGI,KIJITONYAMA JIJINI DAR



MOTO WATEKETEZA GHALA LA KUHIDHIA RANGI,KIJITONYAMA JIJINI DAR
 Askari wa Kikosi cha zima moto wakiendelea na zoezi la uzimaji moto katika ghala la kuhifadhi rangi za kampuni ya Colar Paint lililopo katika Mtaa wa Kenya,Kijitonyama usiku huu.Chanzo cha moto huo hakijafahamika mpaka sasa na eneo kubwa la ghala hilo limeteketea kabisa kwa moto huo.hakuna mtu yeyote alieripotiwa kupoteza maisha au kujeruhiwa katika moto huo.Mpaka Globu ya Jamii inaondoka eneo la tukio,eneo kuwa la moyo huo lililiwa limeshazimwa.

Sehemu ya Maduka yaliyokuwa yamezunguka nje ya ghala hilo kama yanavyoonekana,hakuna alieweza kuokoa chochote.
Maafisa wa vikosi vya zimamoto wakijadiliana jambo mara baada ya kufanikiwa kuzima moto kwa asilia kubwa.