Mbunge wa jimbo la Kigoma kusini David Kafulila amesema wananchi wanataka kuona serikali inawafukuza kazi na kuwafikisha mahakamani vigogo wote waliohusika katika sakata la wizi wa fedha za Tegeta Escrow kwani waliofikishwa mahakamani mpaka sasa ni viongozi wadogo huku vigogo wakubwa wa serikali waliohusika na wizi wa fedha wakipewa likizo ya kutumia fedha hizo.
Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara katika kata ya tungi manispaa ya Morogoro mbunge wa jimbo la Kigoma kusini kwa tiketi ya NCCR mageuzi Davidi Kafurila amesema wananchi wanataka kuona vigogo waliohusika katika sakata la wizi wa fedha za Escrow kufukuzwa kazi, kurejesha fedha hizo na wapelekwe mahakamani na si kuwapeleka watu wadogo huku vigogo wakipewa likizo ya kutumia fedha hizo.
Naye naibu katibu mkuu wa Bawacha taifa kunti Yusufu amewataka wananchi wa Morogoro kuchukua hatua madhubuti juu ya ustawi wa taifa kwa kujitokeza kujiaandikisha katika daftari la kudumu la wapigakura ili kupata fursa ya kuchagua viongozi watakaoweka mbele maslahi ya wananchi na kuwakumbusha wananchi wasidanganyike kupigia kura katiba inayopendekezwa kwani katika hiyo imeweka mbele mashlahi ya vigogo na kuacha kando matatizo ya wananchi.