Thursday, January 08, 2015

MFUMUKO WA BEI WA TAIFA WAPUNGUA KWA ASILIAMIA 4.8 KWA DESEMBA 2014.

 Mkurugenzi wa Sensa na Takwimu,Ephraim Kwesigabo akizungumza na waandishi wa habari hawapo nchini juu mfumuko wa bei kwa desemba mwaka jana.
Meneja wa Utafiti wa Benki Kuu (BoT),Johnson Nyella akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani juu ya sera za Benki Kuu  katika kudhibiti mfumuko.

Na Chalila Kibuda na Globu ya Jamii,Dar.

Mfumuko wa bei  wa  Taifa wa Disemba 2014 ulipungua kwa asilimia 4.8 kutoka   asilimia 5.8 Novemba mwaka jana. Akizungumza na waandishi wa habari leo ofisini kwake Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu Ephraim Kwesigabo alisema mfumuko wa bei kwa mwaka jana ulikuwa imara kutokana uzalishaji mwingi wa vyakula.

Kwesigabo amesema kasi ya upandaji wa bei na bidhaa  na huduma kwa mwaka jana imepungua kwa kasi  ikilinganishwa  mwaka 2013 na fahirisi za bei ziliongezeka disemba mwaka jana kwa kufikia 150.92 kutoka 144.07 mwaka 2013.

Aidha amesema  mfumuko wa bei wa mwezi Desemba,2014 unapimwa kwa kipimo cha mwezi umeongezeka kidogo kwa asilimia 0.2 ukilinganishwa na ongezeko la asilimia 0.6 mwezi Novemba,2014.




Hata hivyo amesema kuwa mfumuko wa bei nchini una mwelekeo unaofanana na baadhi ya nchi nyingine za Afrika Mashariki .