Sunday, January 18, 2015

Matapeli 2 washikiliwa na polisi mkoani Mbeya



Matapeli 2 washikiliwa na polisi mkoani Mbeya
Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Mbeya AHMED MSANGI
Jeshi la Polisi mkoani Mbeya linawashikilia watu wawili wanaodaiwa kuwa ni Matapeli kwa kutumia kivuli cha waganga wa tiba mbadala,baada ya kumtapeli mzee AGOSTINE KADUNDA mkazi wa kijiji cha Igunguli Mtera wilaya ya Dodoma Vijijini.

Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Mbeya AHMED MSANGI amewataja watuhumiwa hao kuwa ni ALEX KAPALANAKA na EFRAHIMU MWAIJEJE wote wakazi wa Mbeya mjini.

Hivi karibuni Mamlaka ya Chakula na Dawa Nchini imekuwa ikitoa elimu juu ya Tiba mbadala, hasa kwa wale wanaofanya uganga kwa kupiga ramuli kwamba hairuhusiwi

Kutokana na tukio hili la utapeli Kamanda Msangi ametangaza oparesheni maalum kwa mkoa mzima wa Mbeya