Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akizungumza jambo na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya chama hicho, January Makamba kwenye Ukumbi wa Kizota Dodoma
Siku chache baada ya matokeo ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa kuonyesha kuwa CCM, imeporomoka, Mbunge wa Bumbuli, ambaye pia ni Naibu Waziri wa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba amewataka wanachama wa chama hicho kujiandaa kisaikolojia kwa matokeo yoyote yanayoweza kutokea katika Uchaguzi Mkuu Oktoba mwaka huu.
"Wana-CCM wanatakiwa kujiandaa kisaikolojia kwani walizoea ushindi wa asilimia 90 au 80 (wa kishindo), huu ulikuwa ushindi wa nyuma. Tusishangae tukipata ushindi wa asilimia 50, 60, 57 au 70 ni kitu cha kawaida kutokana na kukua kwa demokrasia hususan ushindani wa vyama vingi vya siasa kuanza kuimarika.
Kauli hiyo ya Makamba imekuja wakati matokeo ya serikali za mitaa yakionyesha kuwa CCM imeporomoka kutoka ushindi wa asilimia 91.7 mwaka 2009 hadi 79.8 katika uchaguzi wa mwaka jana na upinzani ukipanda kutoka asilimia nane mwaka 2009 hadi takriban 20 mwaka jana.
Akizungumza jana katika mahojiano na kipindi cha 'Power Breakfast' cha Redio ya Clouds na baadaye kufafanua baadhi ya hoja alipozungumza na mwandishi wetu, Makamba alisema matokeo ya uchaguzi huo ni ishara kwamba kwa umri wa miaka 22 sasa, mfumo wa vyama vingi vya siasa umeanza kuimarika.
"Hata ushindi wa asilimia 81 tulioupata katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa bado ni mkubwa na hata kama tungepata asilimia 70 haupunguzi uhalali wa uongozi. Kusema CCM itang'oka madarakani, hapana, bado wananchi wanakiamini tena sana," alisema Makamba.
Makamba ambaye pia ni Naibu Waziri wa Sayansi na Teknolojia, alizungumzia pia namna ya kuwapata wagombea wa urais na kusema mwaka huu ndiyo utapima ukomavu wa chama katika harakati za kumpata mrithi wa Rais Jakaya Kikwete.
Makamba ambaye Julai 2, mwaka jana akiwa London, Uingereza alitangaza nia ya kuwania urais kupitia CCM, alisema mwaka 1995 mgombea alipatikana kwa malezi ya Mwalimu Julius Nyerere, mwaka 2000 aliendelea aliyekuwa
Makamba ambaye Julai 2, mwaka jana akiwa London, Uingereza alitangaza nia ya kuwania urais kupitia CCM, alisema mwaka 1995 mgombea alipatikana kwa malezi ya Mwalimu Julius Nyerere, mwaka 2000 aliendelea aliyekuwapo.po. Alisema mwaka 2005 ilikuwa kama 1995 lakini mwaka huu ni tofauti na vipindi vingine kabisa.
Makamba ambaye Julai 2, mwaka jana akiwa London, Uingereza alitangaza nia ya kuwania urais kupitia CCM, alisema mwaka 1995 mgombea alipatikana kwa malezi ya Mwalimu Julius Nyerere, mwaka 2000 aliendelea aliyekuwapo.po. Alisema mwaka 2005 ilikuwa kama 1995 lakini mwaka huu ni tofauti na vipindi vingine kabisa.
"Hii ni mara ya kwanza hakuna uhakika wa nini kitatokea na kwa mara ya kwanza chama chetu kama taasisi kitajaribiwa... na sisi tuna utaratibu ambao unatakiwa kufuatwa.
"Tuna sifa 13 za kumpata mgombea, sifa hizi na taratibu nyingine zikifuatwa tutampata. Mchakato ukiwa wa haki tutampata kwani nina imani na mwenyekiti (Rais Kikwete), Katibu Mkuu (Abdulrahman Kinana) na Kamati Kuu," alisema Makamba .
Ujana na uzee
Kuhusu hoja ya ujana au uzee ambayo imewagawa wagombea urais wa CCM, Makamba alisema kuna tofauti kati ya umri, uwezo na uzoefu ili wananchi waweze kumwamini mtu na kumpa fursa ya kuwatumikia, jambo ambalo alisema halihitaji kutumia fedha nyingi au kuweka mbele uchu wa madaraka ili kuyafanya mazingira yawe ya lazima kupata.
"Nchi ipo njiapanda na mwaka huu ndiyo itaamua kupaa au kuporomoka lakini kumchangua kiongozi ambaye ameshiriki kuuweka mfumo huu wa uongozi unaolalamikiwa sasa ni kurudisha nyuma maendeleo. Kuna vijana viongozi na viongozi vijana. Kuna vijana ambao wameandaliwa vyema kuja kushika uongozi wa juu, hivyo tukipata viongozi wa sasa wanaojua ulimwengu wa sasa, nchi yetu itaweza kupaa zaidi," alisema Makamba.