Friday, January 09, 2015

klabu za michezo za maveterani Dar es salaam kurehemu marehemu Jumatatu (Mapinduzi Day) Leaders club, Kinondoni, jijini Dar es salaam



klabu za michezo za maveterani Dar es salaam kurehemu marehemu Jumatatu (Mapinduzi Day) Leaders club, Kinondoni, jijini Dar es salaam
Umoja wa klabu za michezo za maveterani Dar es salaam,  chini ya uratibu wa klabu za Singasinga na Tazara,  unatangaza rasmi kwamba  shughuli ya kurehemu wanachama wenzetu ambao wametangulia mbele ya haki itafanyika JUMATATU 12/1/2015, ikiwa pia ni  sehemu ya kuadhimisha sikukuu ya Mapinduzi.

Ratiba itaanza  Saa 7 mchana katika viwanja vya Leaders club jijini Dar es salaam. Dua zitafanyika  kutoka kwa Father Oscar na Sheikh Kipoozeo. Dua hizo zitafuatiwa na Chakula cha pamoja cha mchana kitachoandaliwa na Mpishi maarufu nchini, Chef  Saidi Bajia,  na  baadae burudani mbalimbali za  nguvu zitaendelea. 

Karibuni tujumuike wote... 

Pichani chini ni shughuli kama hii zilizofanyika miaka iliyopita.
- Imetolewa na Balozi Cisco Mtiro, Mratibu mkuu wa shughuli hii.
wanachama wa klabu za michezo za maveterani Dar es salaam wakiwa katika shughuli hiyo ya kuwakumbuka wenzao miaka ya nyuma
Mapochopocho
wadau
Kila mtoto wa mujini alikuwepo
Vilaji