Sunday, January 04, 2015

JK AKIREJESHA KIWANDA CHA CHAI CHA MPONDE LUSHOTO KWA WANANCHI


JK AKIREJESHA KIWANDA CHA CHAI CHA MPONDE LUSHOTO KWA WANANCHI
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, akihutubia katika mkutano ulioandaliwa rasmi kuwaambia wananchi wa Mponde, Halmashauri ya Wilaya ya Bumburi, Lushoto mkoani Tanga, kuwa Rais Jakaya Kikwete amekubali kukirudisha Kiwanda cha Chai cha Mponde kwa wananchi baada ya mgogoro dhidi mwekezaji wa kiwanda hicho, Yusufu Mula uliodumu kwa takribani miaka 10 na kusababisha kiwanda hicho kufungwa maiaka miwili iliyopita na kuwaacha wananchi kwenye lindi kubwa la umasikini.

Hayo ni Mafanikio ya Katibu Mkuu wa CCM,  Abdulrahman. Kinana ambaye katika mkutano wa hadhara uliofanyika Septemba mwaka jana katika Kijiji cha Mponde, aliahidi kupata suluhu ya mgogoro wa kiwanda hicho ulioshindikana kutatuliwa kwa muda mrefu kwa kuupeleka kujadiliwa katika Kamati Kuu ya CCM na kupata ufumbuzi ndani ya mwezi mmoja, ahadi ambayo aliitimiza.

Kiwanda hicho kilifungwa baada ya wananchi kususia kuendelea kulima mashamba ya chai kwa lengo la kuishinikiza Serikali kutatua haraka mgogoro dhidi ya Mwekezaji wa kiwanda hicho, Yusufu Mulla, ambaye walidai kuwa alikuwa anawanyanyasa wakulima wa zao hilo pamoja na wafanyakazi kuwalipa ujira mdogo.

Kinana amesema Serikali itanunua hisa za mwekezaji ili aondoke na kuwaachia wananchi kiwanda hicho.Pia Serikali itatuma jopo la wataalamu watakao tathmini hasara iliyopo, na kutafuta mtaji wa kukifufua kiwanda  ili kianze kufanya kazi
Mbunge wa Jimbo la Bumbuli,Mh. January Makamba akiishukuru Serikali kwa uamuzi wake wa kukirudisha kiwanda hicho kwa wananchi ambapo pia alimshukuru Rais Jakaya Kiwete na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman kwa kufanya jitihada za kuhakikisha wananchi wanapata haki yao hiyo walioisotea kwa takribani miaka 10.

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Mbunge wa jimbo la Bumbuli Mh. Januari Makamba wakati alipowasili jimboni humo katika wilaya ya Lushoto, akiwa katika ziara ya siku mbili ambapo amefanya mkutano wa hadhara katika kata ya Mponde na kuwataarifu wananchi na wakulima wa Chai kuhusu maagizo ya Rais Jakaya Kikwete juu ya kukirejesha kiwanda cha Chai cha Mponde kwa wananchi .
  Baadhi ya Wananchi waliojitokeza kwa wingi kwenye mkutano huo wa hadhara wakisikiliza kwa makini. 
 Wananchi wa Bumbuli wakifuatilia mkutano wa hahara.
 Mkutano ukiendelea katika uwanja wa Mponde,katika Halmashauri ya Bumbuli mkoani Tanga jioni ya leo.
 Mkuu wa Wilaya ya Lushoto,Mh.Majid Hemed akizungumza na Wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika jioni ya leo katika kijiji cha Mponde,mkoani Tanga.
 Baadhi ya Wananchi waliojitokeza kwa wingi kwenye mkutano huo wa hadhara wakisikiliza kwa makini
 Mmoja wa Wananchi akishangilia kwa namna yake mara baada ya Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana kutamka kuwa kiwanda cha Chai cha Mponde Rais Kikwete ameamuru kilejeshwe mikononi mwa Wananchi na Wakulima wa Chai. 
 Wananchi wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye mkutano huo.
 Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Magalulla Said Magalulla akiwasalimia na kujitambulisha kwa wakazi wa Bumbuli na Vitongoji vyake,kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika jioni ya leo katika uwanja wa Mponde,Mkoani Tanga.
 Mbunge wa Jimbo la Lushoto na Mwenyekiti wa CCM Mkoa Tanga,Henry Shekifu akifafanua jambo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika leo katika uwanja wa Mponde,Mkoani Tanga.