Na Bashir Yakub
Katika shughuli zetu za kuuza na kununua ambazo tunazifanya kila siku mikataba ya maandishi ni jambo ambalo wengi tunakutana nalo. Mikataba hii iwe rasmi au isiwe rasmi suala la msingi ni kuwa huwa tunaifanya. Aidha wakati mwingine si wote wenye kuhusisha suala la mikataba ya maandishi katika makubaliano yao mbalimbali na hii hutokana na sababu mbalimbali ikiwemo ya kuaminiana. Kuhusu kuaminiana niseme jambo moja tu kuwa suala la mikataba ni muhimu sana hata kana mwenzako unamuamini kwa kiwango cha juu kabisa( highest degree of trust).
Nathubutu kusema kuwa hata awe mzazi wakokama kuna jambo la msingi mmelifanya ni vema kukawapo mkataba wa maandishi. Nasema hivi kwakuwa kwa uzoefu wangu wa mambo haya mara nyingi mgogoro hautokani na waliouziana au kukubaliana isipokuwa mgogoro unakuja kuanzishwa na walio nyuma ya hao.
Kwa mfano baba anaweza kumpa mwanae kiwanja na wasifanye mkataba wowote wa maandishi kwa kuwa wanaaminiana. Hiyo ikaenda kwa miaka kadhaa ambapo baba akawa amefariki. Baaada ya hapo anaibuka mtu anasema mimi ni mtoto wa marehemu kwa hiyo nahitaji kiasi kadhaa kutokamali hii.
Hapa mgogoro si kati ya baba na mwana tena isipokuwa ni kati ya mwana na mtu mwingine.Kama huna mkataba wowote wa maandishi mpaka kesi hii kuisha waweza kuwa umepoteza kila kitu. Huu ni mfano tu katika kusisitiza kuwa mtu asiseme mi na fulani tunaaminiana. Mgogoro sio lazima utokane na nyie wawili isipokuwa walio nyuma yenu waweza kuanzisha mgogoro.
Nathubutu kusema kuwa hata awe mzazi wako
Kwa mfano baba anaweza kumpa mwanae kiwanja na wasifanye mkataba wowote wa maandishi kwa kuwa wanaaminiana. Hiyo ikaenda kwa miaka kadhaa ambapo baba akawa amefariki. Baaada ya hapo anaibuka mtu anasema mimi ni mtoto wa marehemu kwa hiyo nahitaji kiasi kadhaa kutoka
Hapa mgogoro si kati ya baba na mwana tena isipokuwa ni kati ya mwana na mtu mwingine.
MADHARA YA KUTOFANYA MKATABA WA KISHERIA .
Ni vema sana kujihadhari kwakuwa ukisikia neno mgogoro ujue kuna mambo makubwa mawili. Kwanza gharama kubwa ni uwezekano wa kupoteza kabisa ile mali na haijalishi iwe uliinunua au ulipewa isipokuwa tu ukishakuwa na mgogoro upo katika hatari hiyo. Pia gharama ya pesa kama kuwalipa wanasheria, gharama za uendeshaji kesi, nauli na matumizi mengineyo ambayo hujitokeza bila hata kutarajia. Pili kuna gharama ya muda .
Hii huhusisha kushinda mahakamani kila siku na wote mwajua mahakama zetu zilivyo, kushinda vituo vya polisi huku shughuli zako za msingi za kila siku zikisimama. Pia hapa kuna muda wa kusubiri hukumu ambapo kesi yaweza kukaa mahakamani hata miaka sita . Hakika unakuwa umesurubika(suffer) na umepoteza mambo mengi katika kushughulikia jambo hili.
Hii huhusisha kushinda mahakamani kila siku na wote mwajua mahakama zetu zilivyo, kushinda vituo vya polisi huku shughuli zako za msingi za kila siku zikisimama. Pia hapa kuna muda wa kusubiri hukumu ambapo kesi yaweza kukaa mahakamani hata miaka sita . Hakika unakuwa umesurubika(suffer) na umepoteza mambo mengi katika kushughulikia jambo hili.
USHAURI.
Ushauri wa kawaida tu kwa hili ni kuwa na utamaduni wa kuweka katika maandishi kila makubaliano na hii iwe kwa watu wote mnayeaminiana sana au msiyeaminiana. Fanya hili kuwa utamaduni wako kwa kuweka kila muamala wako katika maandishi suala la kuaminiani lisiwe hoja tena kwakuwa mgogoro hautakuwa kati yako na yeye isipokuwa unaweza kuwa kati ya mtu wa nyuma yake na wewe au mtu wa nyuma yako na yeye. Nitatoa mfano mwingine halisi ambapo mfano huu ni kesi ipo mahakamani hadi leo.
Mwaka 2010 mwezi wa saba mtu mmoja alimuuzia rafiki yake gari aina ya land cruiser akiwa anatafuta fedha kwa ajili ya safari yake ya uingereza baada ya kupata kazi huko. Wakauziana na kwakuwa waliaminianasana hawakuandikishana popote.
Mwaka mmoja na nusu baadae gari hiyo ikakamatwa maeneo ya Sinza na polisi kwasababu kuwa mwaka 2009 Disemba iliwagonga watu wawili na kuuwa mmoja maeneo ya tabata na kukimbia. Mnunuzi alijitetea kwa urahisi tu kuwa gari amelipata 2010 July kwa hiyo hawezi kuwa anahusika na lolote kabla ya muda huo.
Utetezi wake ulikubaliwa isipokuwa tu alitakiwa atihibitishe kwa kuonesha mkataba halali wa mauziano ambao utaonesha kuwa ameanza kumiliki garihilo baada ya ajali. Ilikuwa vigumu kwake na hilo likamwingiza moja kwa moja katika kesi hiyo na mpaka naandika makala haya amesota na kesi hiyo kwa miaka minne sasa na haijajulikana inaisha lini ambapo kwa mtazamo wa kitaalam kuna uwezekano mkubwa wa kupatikana na hatia na kwenda jela.Kwa hiyo utaona hapa kuwa kufanya maandiko ya kisheria katika kila muamala si muhimu tu katika kudhulumiana bali pia hata mambo mengine kama haya ambayo yanaweza kujitokeza bila kutarajia.
Mwaka 2010 mwezi wa saba mtu mmoja alimuuzia rafiki yake gari aina ya land cruiser akiwa anatafuta fedha kwa ajili ya safari yake ya uingereza baada ya kupata kazi huko. Wakauziana na kwakuwa waliaminiana
Mwaka mmoja na nusu baadae gari hiyo ikakamatwa maeneo ya Sinza na polisi kwasababu kuwa mwaka 2009 Disemba iliwagonga watu wawili na kuuwa mmoja maeneo ya tabata na kukimbia. Mnunuzi alijitetea kwa urahisi tu kuwa gari amelipata 2010 July kwa hiyo hawezi kuwa anahusika na lolote kabla ya muda huo.
Utetezi wake ulikubaliwa isipokuwa tu alitakiwa atihibitishe kwa kuonesha mkataba halali wa mauziano ambao utaonesha kuwa ameanza kumiliki gari
JE KILA MAANDISHI NI MKATABA.
Aidha uandishi mzuri wa mkataba wa kisheria hupelekea mkataba wenye hadhi na mkataba wenye hadhi ndio mkataba halali ambao hukubalika kisheria na pia huweza kutumika kama ushahidi endapo kuna tatizo. Yawezekana unao mkataba lakini hauna hadhi kisheria na likijitokeza jambo mkataba wako hautakubalika. Si kila maandishi ni mkataba isipokuwa mkataba huwa na vitu maalum vya kisheria ambavyo huufanya kukubalika na kutambuliwa. Haya hapa ndio mambo ya msingi ambayo hutakiwa kuwa ndani ya mkataba.
MKATABA MZURI HUWA NA HAYA :
( a ) Lazima uwe na majina ya wahusika ambayo yatakuwa yameandikwa kwa urefu na kwa kueleweka.Mfano jina liwe Paschal Mayenge Archard. Epuka kuandika vifupi mfano P.M. Archard. Jina linatakiwa liwe katika ukamilifu wake na hasa pawe na majina matatu kamili. Pia majina ya pande zote mbili yaani muuzaji na mnunuzi yatokee hivyohiyvo si tu majina ya upande mmoja. Yawezekana mkataba mwingine unahusisha watu wengi zaidi pia ni muhimu majina matatu ya kila mmoja yaonekane hata kama wako ishirini.
( b ) Katika majina hayo hadhi ya kila mmoja iainishwe mbele ya jina lake. Mfano kama ni muuzaji au mnunuzi mbele iandikwe kuwa huyu ni muuzaji na huyu ni mnunuzi. Halikadhalika kama ni mkopaji, mkopeshwaji, mtoa zawadi mpokea zawadi viainishwe.
( c ) Bei au gharama halisi ya mauziano ioneshwe. Iandikwe kwa tarakimu yaani namba mfano 1,000,000/= na kwa maneno katika mabano ( Milioni moja tu).Ni muhimu yote mawili yaonekane , hii huondoa utata.Tarehe ya mkataba ioneshwe sambamba na maelezo kama fedha imelipwa yote au kiasi.
( d ) Kama kuna kiasi kilichobaki kianishwe kwa tarakimu na pia kwa maneno kama nilivyoonesha hapo juu. Muda wa kulipa kilichobaki nao uainishwe ikiwa ni pamoja na hatua za kuchukua ikiwa muda uliowekwa utapita. Mkataba lazima uoneshe muda ukipita nini kifanyike mfano ikifika tarehe 7. 12. 2015 saa kumi jioni kiasi cha pesa iliyobaki hakijalipwa basi mali itamrudia mwenye nayo na mnunuzi hatakuwa na deni lolote dhidi ya muuzaji, au itahesabika kuwa mkataba umevunjika na mnunuzi atatakiwa kumlipa fidia ya kiasi fulani muuzaji kwa kuvunja mkataba.
( e )Mashahidi ni muhimu kila upande. Kila upande hata ukiwa na shahidi mmoja wala si mbaya. Shahidi awe mtu wa kuaminika , mtu mzima na mwenye akili timamu. Wataandika majina yao matatu kwa urefu kama yalivyo ya wahusika na pia wataweka sahihi zao huku ikioneshwa shahidi yupi wa upande upi na yupi wa upande upi. Wakili ni mtu muhimu sana kwa wakati huu kwani wakili anaweza kuwa shahidi pekee bila kuwapo shahidi mwingine yeyote.
Wakili anakuwa shahidi wa wote wawili na panakuwa hapahitajiki mwingine yeyote.Pia wakili ni shahidi wa kuaminika zaidi na anaaminiwa na kila mamlaka ikiwemo mahakama na hivyo uwepo wake katika mkataba ni ulinzi tosha kwa mkataba wako.
Wakili anakuwa shahidi wa wote wawili na panakuwa hapahitajiki mwingine yeyote.Pia wakili ni shahidi wa kuaminika zaidi na anaaminiwa na kila mamlaka ikiwemo mahakama na hivyo uwepo wake katika mkataba ni ulinzi tosha kwa mkataba wako.
( f ) Mali inayouzwa au iliyohusishwa kwenye mkataba ichambuliwe vyema. Kama ni kiwanja au nyumba ielezwe mtaa, kata, tarafa kitongoji,mkoa,plot namba kama ipo, urefu, upana, ikiwezekana jirani wa kushoto na kulia.au magharibi, mashariki, na kama ni gari, pikipiki maelezo yote yaliyo kwenye kadi yaingie katika mkataba ili kutambua kwa undani mali yenyewe.
( g ) Anuani za muuzaji au mnunuzi ziwepo ikiwa ni pamoja na namba ya simu. Hili la namba ya simu ni muhimu sana kwasasa kutokana na msaada mkubwa wa mawasiliano haya endapo mtu atahitajika.
( h ) Picha ndogo yenye kuonesha taswira ya mtu kwa ukamilifu (passport size) ni muhimu sana na ibandikwe mbele ya jina la mtu. Si muhimu sana kwa mashahidi lakini kwa wahusika wenyewe ni muhimu sana .
( I ) Alama ya dole gumba mbele ya jina nayo ni muhimu sana . Hii ni kutokama na alama hii kutoweza kwa namna yoyote kuingiliwa au kughushiwa.Tia dole kwenye kablasha ya muhuri na weka dole gumba mbele ya kila jina. Hii pia si lazima kwa mashahidi.
( j ) Kama ni kiwanja au nyumba ni muhimu mkataba uoneshe kama kimelipiwa kodi ya ardhi ( Land rent) na kama hakijalipiwa mkataba ueleze nani atalipa kodi hiyo kati ya anayenunua au anayeuza.
( k ) Pia ni muhimu sana mkataba uoneshe iwapo mgogoro wowote utatokea kuhusiana na mkataba huo nini wahusika wafanye, mfano endapo mgogoro utatokea kuhusiana na mkataba huu mahakama ya Tanzania yenye mamlaka ndio itahusika na utatuzi wa mgogoro. Sambamba na hilo mkataba uweke wajibu kwa muuzaji kuwa tayari kumpa ushirikiano mnunuzi iwapo mali aliyomuuzia itaonekana kuwa na mgogoro mbeleni mfano muuzaji atampa ushirikiano mnunuzi endapo kutatokea mgogoro wowote kuhusiana na mauziano haya.
Kwa ufupi hayo ni baadhi tu ya mambo ya msingi katika kukufanya kuwa salama katika mikataba. Nirudie tu kusema kuwa si kila maandishi uliyoandika na kuhifadhi nyumbani kwako ni mkataba jitahidi kuwa na mkataba wa kisheria.
Mwandishi wa makala haya ni Mwanasheria na Mshauri wa sheria kupitia gazeti la serikali Habari Leo kila jumanne, gazeti Jamhuri kila jumanne na Nipashe jumatano.
0784482959
0714047241